Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo,Kamisha Suleiman Kova
Kanisa
Katoliki Parokia ya Makoka limefichua siri kuhusu mauaji ya Sista
Cresensia Kapuli (50), aliyeuawa na majambazi kwa kupigwa risasi kwamba
alifikwa na mauti hayo wakati akitoka benki kuweka fedha za sadaka
ziliyopatikana Jumapili iliyopita.
Mwenyekiti wa Parokia hiyo, John Bosco Komba, aliliambia NIPASHE jana
kuwa sista huyo aliuawa baada ya kutoka benki ya CRDB tawi la Mlimani
City kuweka fedha za sadaka na makusanyo ya Shule ya Sekondari ya
Mwenyeheri Anuarite.
“Taarifa zilizoripotiwa na vyombo vya habari kwamba ameporwa fedha
zinaweza zisiwe na uhakika sana kwa sababu alitoka benki kuweka fedha za
makusanyo ya sadaka, ndipo akapitia kununua mchele zaidi ya kilo mbili
kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kwa hiyo hakuwa na fedha nyingi kama
inavyoelezwa na watu,” alisema.
Komba alisema Sista Kapuli mbali na kuwa mhasibu wa shule,pia alikuwa
mhasibu wa Kanisa Katoliki Parokia ya Makoka na kwamba siku ya tukio
alikuwa na mwenzake Sista Brigitha ambaye ni Mwalimu Mkuu msaidi wa
Shule ya Sekondari Mwenyeheri inayomilikiwa na kanisa hilo.
Alisema walipofika katika duka walilokwenda kununua mchele Sista
Brigitha ndiye aliyetelemka kwenye gari kwenda kununua na ndipo ghafla
majambazi wawili waliokuwa katika pikipiki walitokea na kupiga risasi
moja iliyovunja kioo cha gari ambayo ilimjeruhi dereva wa gari hilo,
Mark Patrick Mwarabu.
Aliongeza kuwa majambazi hao walidhani kuwa mkoba aliokuwa nao
ulikuwa na fedha nyingi walimpiga risasi mbili Sista Kapuli eneo la titi
upande wa kushoto na kufa papo hapo.
Alisema madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
wataufanyia uchunguzi mwili wa Sista Kapuli leo kwa ajili ya kumuondoa
risasi kabla ya taratibu za kuusafirisha mwili huo kuupeleka kwao katika
kijiji cha Mkulwe wilayani Mbozi, mkoani Mbeya.
Alisema baada ya taratibu za uchunguzi wa mwili huo kufanyika, kesho
mwili utapelekwa katika Kanisa la Makoka kwa ajili ya misa na kuuaga na
safari ya kuusafirisha kwenda kijijini kwao wilaya ya Mbozi itaanza huku
akisema kifo hicho kimewasikitisha.
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limetangaza kuanza
kwa msako ili kuwabaini na kuwakamata majambazi waliohusika katika tukio
hilo.
Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Kamisha Suleiman Kova, alisema jana
kuwa Jeshi lake limeandaa operesheni maalumu itakayohusisha vikosi
tofauti ili kuwatia mbaroni wahalifu hao, ambao alisema walipora Sh.
milioni 20
Post a Comment