Hatimaye
mwanadada Jacqueline Wolper ameamua kuweka wazi kilichotokea mpaka
kuamua kubadili Dini yake ya Uislamu na kurudi kwenye ukristo tena.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii mwanadada huyu wa bongo movies ametoa ujumbe ufuatao kwa mashabiki wake.“…mambo
mashabiki zangu.sikua na njia nyingne yakulikwepa hili nanaamini kua
kwa wale mashabk zangu waislam amtomaind maana akuna mtu wakumsikiliza
chin ya hanga zaidi yawazazi so imenipasa kurudi kanisani kwakauli
yawazazi wangu.naamin kama aujaolewa ata uwe na miaka
mingap bado unatakiwa kua chin ya imaya ya wazazi ata ukifa ujue
unazikwaje na mimi ni binadam sijui saa wala dakika.muhm nikuwajuza
nakuwaelewesha mashabk zangu stak maswal nawapenda wote…”
Hapo
awali iliripotiwa kuwa mwanadada huyu ameamua kuwa mkristo tena baada
ya penzi lake lililosababisha abadili dini na kuwa muislamu na jamaa
aitwaye 'Dallas' kuvunjika hivi karibuni.
Post a Comment