Mwanamuziki Diamond amefunguka kuhusu madai ya baadhi ya wasanii kuwa aliwaibia idea au nyimbo zao na kuzifanya zake.Ameeleza
kuwa malalamiko yao hayana ukweli kwa kuwa kuna maneno ambayo
yamezoeleka na yanaweza kutumiwa na watu wote lakini anapoyatumia
hutokea msanii aliyetumia maneno kama yale na kudai kuwa ameiba idea
yake.
Ametoa
mfano wa nyimbo kama Moyo Wangu ambao anasema baada ya kuimba wasanii
wengine waliimba pia lakini hakuwahi kujitokeza kusema ameibiwa kwa
sababu neno hilo linaweza kutumika na kila mtu kwa ufundi wake. Diamond
ameeleza pia kuhusu tuhuma za Wababa (ingawa hakumtaja jina) kuwa
alimuibia wimbo wake wa Kitorondo na sasa anauita Mdogomdogo.
“Sitaki
niongee kwa sababu nitampa Kick…anyways nilisikia kuna mtu anasema eti
hii nyimbo yangu ya MdogoMdogo kuna mtu kaibiwa kwa neno la Kitorondo.
Sasa mimi nikuadithie story fupi…mimi nimezaliwa Tandale nimekulia
Tandale, kuna bendi ilikuwa inaitwa Tandale Modern Taarab nyimbo yao ya
kwanza inaitwa Tandale (anaimba kidogo). Ukiacha hivyo, Kitorondo ni
jina ambalo ni ngoma ambayo wanaimba hivyo (anaimba). Yaani hii ni
nyimbo.
“Kuna
msanii kaichukua kaiimba kama ilivyo ile nyimbo ya mdundiko. Halafu
baada ya kusikia neno la Kitorondo kwenye nyimbo yangu akasema yeye
kaibiwa nyimbo. Mimi nimepata taarifa nikasema ana akili kweli. Yeye
ndio kaenda kuiba. Mimi nimetumia neno la Kitorondo kwa taaluma zangu za
kimuziki naliingiza kwa namna gani kama neno, yeye anasema nimemuibia
yeye. Sikujisikia vizuri…halafu nikaulizwa kila sehemu nikienda
nawaambia msiniulize maswali hayo kabisa.”
Chanzo Bongo clan
Post a Comment