LUIS
Suarez amekiri kuwa magoli yake mawili ambayo yamewaacha England njia
panda katika fainali za kombe la dunia ni kisasi kitamu kutokana na
ukosoaji waliofanya juu yake wakati anacheza ligi kuu ya nchi hiyo.
Nyota
huyo wa Uruguay na Liverpool alifungiwa kwa kumfanyia ubaguzi wa rangi
beki wa kushoto wa Ufaransa na Manchester United, Patrice Evra. Pia
kitendo chake cha kumung`ata kwa meno beki wa Chelsea, Branislav
Ivanovic kilimufanya afungiwe katika msimu wa utata kwake nchini
England.
Baada
ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya England, Suarez, ambaye alicheza mechi
yake ya kwanza tangu afanyiwe upasuaji wa goti alisema: “Niliota jambo
hili, Nafurahia muda huu, kwasababu ya yote niliyoumia, ukosoaji
niliopokea. Kwahiyo, mnaondoko.”
Suarez, ambaye alikosa mechi ya ufunguzi ya Uruguay akishangilia bao la kwanza Sao Paulo
Shangwe: Akishangilia baada ya kufunga bao la pili Sao Paulo.
Suarez
aliongeza: ‘Kabla ya mchezo watu wengi nchini England walicheka
matatizo yangu miaka michache iliyopita. Huu ni muda mzuri kwangu.
Nataka kujua sasa wanawaza nini”.
“Ulikuwa mchezo mzuri niliowahi kucheza. Ni muda wa ajabu kwangu. Labda siku mbili zilizopita sikuwaza kama ingewezekana”.
Suarez alifunga bao la ushindi dakika tano kabla ya mpira kumalizika baada ya Wayne Rooney kusawazisha bao la kwanza.
Post a Comment