Mtoto Samson Matei Joseph akiwa na baba yake mzazi, Bw. Matei Joseph.
Mtoto aliyezaliwa na wazazi wa kabila la Kingoni (Mngoni), Samson Matei Joseph wa Nguruka Kata ya Nguruma wilayani Uvinza mkoani Kigoma alipotea miaka miwili iliyopita lakini katika hali ya kushangaza, hivi karibuni ameibuka akiwa ni Mmasai baada ya kusakwa bila mafanikio.
Akizungumza
na paparazi kwa njia ya simu akiwa mkoani Kigoma, baba mzazi wa mtoto
huyo, Matei Joseph alisimulia mkasa mzima na kusema kuwa yeye na mkewe
walimpoteza mtoto wao huyo Desemba 16, 2012 wakati huo akiwa na umri wa
miaka 11, akisoma darasa la tatu.
Alisema kuwa baada ya kupotea walimsaka kila kona ya nchi bila mafanikio na kuamua kumuachia Mungu.
“Siku
moja niliona simu yangu ya mkononi ikiita kwa namba ngeni, nilipopokea
kuna bibi kajitambulisha kwa jina la Mama Vero akasema kuna mtoto
anataka kuongea na mimi.
“Alimpatia simu mtoto ambaye alijitambulisha kuwa yeye ni Samson, nilifurahi na kushangaa lakini pia sikuamini kwani alikuwa akiongea Kimasai!” alisema Matei.
“Alimpatia simu mtoto ambaye alijitambulisha kuwa yeye ni Samson, nilifurahi na kushangaa lakini pia sikuamini kwani alikuwa akiongea Kimasai!” alisema Matei.
Matei
alisema mwanaye huyo alimwambia kuwa alikuwa Chalinze mkoani Pwani
akihitaji msaada, akilalamika kuteswa kwa muda mrefu na Wamasai ambao
ndiyo waliomtorosha.
“Nilifunga safari hadi Chalinze na kukuta kweli ni Samson, lakini alikuwa katika muonekano wa Kimasai kwani aling’olewa meno nane kama mila zao zinavyosema,” alisema Matei.
“Nilifunga safari hadi Chalinze na kukuta kweli ni Samson, lakini alikuwa katika muonekano wa Kimasai kwani aling’olewa meno nane kama mila zao zinavyosema,” alisema Matei.
Aliendelea
kusimulia kwamba alipomhoji mwanaye alidai alichukuliwa na Mmasai
aliyemtaja kwa jina moja la Samson ambaye alikuwa akiuza dawa na pipi
mkoani Kigoma kabla ya kumuiba na kutimkia naye Chalinze.
“Nilishangaa kusikia alichukuliwa na Mmasai niliyekuwa namjua ambaye alikuwa akifanya biashara pale Nguruka huku Kigoma.
“Alimrubuni
mwanangu kuwa anakwenda kufanya kazi dukani kwa mama Yoyoo, kumbe ni
kuchunga ng’ombe na mabwawa ya maji,” alisema Matei.
Baada ya kupata habari kamili, Matei alikwenda Kituo cha Polisi cha Nguruka na kutoa taarifa ambapo alifungua jalada la kesi namba NGK/IR/2022/2014- KUTOROSHA MTOTO.
Baada ya kupata habari kamili, Matei alikwenda Kituo cha Polisi cha Nguruka na kutoa taarifa ambapo alifungua jalada la kesi namba NGK/IR/2022/2014- KUTOROSHA MTOTO.
“Baada
ya kuchukua RB niliambiwa nifanye juu chini nikamfuate mwanangu
Chalinze kisha nimtafute Nasoro kwa ajili ya kumfungulia kesi ya kujibu.
“Kweli nilifanya hivyo, tulipomkamata Nasoro hakuwa na la kujibu, nikamchukua mwanangu nikarudi naye Kigoma,” alisema Matei.
“Kweli nilifanya hivyo, tulipomkamata Nasoro hakuwa na la kujibu, nikamchukua mwanangu nikarudi naye Kigoma,” alisema Matei.
Kwa
upande wake mtoto Samson alisema kuwa alikuwa amewekwa kwenye mapori ya
Milima Mitatu Chalinze Kata ya Vizimbwi ambapo alikuwa akichunga
ng’ombe na mabwawa ya maji.
Alisema
alifanikiwa kutoroka baada ya kuua sungura na kuwauzia Wamasai wengine
ambapo alipata fedha ndipo akakutana na Mama Vero ambaye alimnunulia
vocha akawapigia wazazi wake kwa kuwa alikuwa akikumbuka namba zao
kichwan
Post a Comment