Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Makamu wa Rais wa China atembelea Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA).



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao (kulia) akiangalia jengo la Makao Makuu ya Ofisi ya Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya shirika hilo leo jijini Dar es Salaam kwenda kuangalia miundo mbinu ikiwemo mabehewa na injini za treni za shirika hilo.  
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao (kushoto) akiangalia ramani ambayo reli ya TAZARA inapita kuanzia kituo cha Dar es Salaam wakati alipotembelea Makao Makuu ya Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia miundo mbinu ikiwemo mabehewa na injini za treni za shirika hilo. Kulia ni Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Harrison Mwakyembe.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao (katikati) akielekea katika moja ya treni ya Shirika la Reli la TAZARA kwa ajili ya kuelekea katika moja ya kituo cha Mizigo cha treni ya TAZARA kilichopo Yombo jiji Dar es Salaaam.
 Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa amekaa ndani ya moja ya treni ya abiria tayari kuelekea katika kituo cha Mizigo cha treni ya TAZARA kilichopo Yombo jiji Dar es Salaaam. Kulia ni mgeni wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao.
 Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Harrison Mwakyembe akishuka toka ndani ya treni ya abiria ya TAZARA kuelekea katika kituo cha mizigo cha TAZARA kilichopo mtaa wa Yombo jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao akishuka toka ndani ya treni ya abiria ya TAZARA kuelekea katika kituo cha mizigo cha TAZARA kilichopo mtaa wa Yombo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupatiwa maelezo ya kina kuhusiana na reli hiyo
 Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Harrison Mwakyembe (kushoto) akimpa maelezo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao (kulia) kuhusiana na shughuli zifanywazo na kituo cha kuhifadhia mizigo inayobebwa na treni ya Shirika la TAZARA wakati alipotembelea katika kituo hicho leo jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao (kushoto) akimshukuru Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Harrison Mwakyembe (kulia) mara baada ya kupata maelezo mazuri kuhusu kazi zifanywazo na Makao Makuu ya Shirika la TAZARA.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao (wa pili toka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na mwenyeji wake Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Harrison Mwakyembe (kulia) mara baada ya kukamiliha ziara ya kutemebelea Makao Makuu ya Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) leo jijini Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top