June 20 2014 Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ni miongoni mwa
waliowasha vipaza sauti kwenye bunge la bajeti linaloendelea Dodoma ambapo sehemu ya alichochangia ni hiki kinachofata
hapa chini.
‘Dola bilioni moja miaka kumi nyuma ilikua ni Trilioni 11 lakini sasa
unaongelea Trilioni 17 kwa hiyo shilingi imeshuka thamani lakini
unashangaa kwanini tunaendelea kuongeza ushuru kwenye pombe na sigara
kama chanzo cha mapato ya taifa letu, nchi nyingi duniani zinazoongeza
ushuru kwenye pombe na sigara lengo lake ni kuona idadi ya wanaokunywa
na kuvuta inapungua tofauti na Tanzania ambako lengo limekua ni
kukusanya mapato, hiki ni kitu cha kusikitisha sana’
‘Nimekwenda Singida hivi karibuni kwenye ziara ya chama chetu na Mh.
Tundu Lissu, ukiwa Singida na Dodoma unaona kuna jua kali… Singida Same
serikali imeweka vikao barabarani >> NENDA POLEPOLE HAPA KUNA
UPEPO MKALI UNAUA << ingekua ni taifa kama Israel, upepo mkali
hauwekewi vibao vya kuua bali upepo mkali unachukuliwa kuwa umeme’
‘Sehemu kubwa ya Singida na Dodoma ni semi desert, serikali ingeweza
kabisakabisa kutengeneza solar village maeneo haya ikatengeneza umeme
mkubwa kupitia nguvu za jua ukaingiza kwenye gridi ya taifa na mngeweza
kupunguza bili za umeme ambazo Wananchi kwa sasa wanapigwa huko mitaani’
‘Hata
kama kutakua na mpango wa aina gani, unapokua na serikali ambayo
haifikirii kwa upana… serikali ambayo inasema bado inakopesheka, bado
tunaweza kukopesheka…. mimi ningekua ni nyinyi, ningekwenda kukopa
barabara zote nchi nzima zijengwe, ningeenda kukopa reli ijengwe,
ningekwenda kukopa Airport ziboreshwe na ningekwenda kukopa serikali
yenu ihamie hapa Dodoma’
‘Watu wengi wamesema kuhusu serikali kuhamia hapa Dodoma, ukiondoa
serikali Dar es salaam ukaileta Dodoma utaipa nguvu hii Ruaha ambayo
hakuna watalii, watalii wataanza kwenda kwa sababu wakuu wote wa nchi
watakuwa wanakuja Dodoma kufanya mikakati yao kwa hiyo centre ya
mapumziko itakua ni Iringa, Mbeya na Singida hapa’
‘Mimi ningekua nyinyi ningefanya maamuzi magumu, ningechukua Mawaziri
wote na makatibu wakuu wote waje hapa wakae gesti na wengine wakae
kwenye matent kwa sababu msipochukua maamuzi serious hamuwezi kuibadili
hii nchi, hii nchi haitobadilishwa kwa Kinana kuzunguka kutafuta kura za
Urais huko kote anakokwenda’
1 comments:
Hapo ndipo inapojidhihirisha kuwa sisi wapiga kura tunakazi kubwa ya kuwapima wawakilishi wetu kwa michango yao wanayoitoa kama inaonyesha uwezo wao wa kiakili, busara na hekima ya kuzaliwa nayo! Aina ya maoni hayo inatupa mashaka kuwa kama tumemchagua mwakilishi mwenye kustahili kwa maendeleo yetu! au anazungumza tu ili asikike japo anachokizungumza ni sawa na mtoto anayejifunza kuongea? Kwani huwa watoto wana maswali mengi mengine ya kuchekesha!! Kufanya kosa si kosa bali kurudi kosa ni kosa! Tutafakari kabla ya kuchagua
ReplyPost a Comment