Martha
John katikati akiwa na washindi wa nafasi ya pili na ya tatu baada ya
kutangazwa mshindi wa taji la Redds Miss Iringa 2014 jana katika
ukumbi wa St Dominic huku mshindi wa pili ni Elizabeth Titus na
mshindi wa tatu ni Fowe Mkuchu(picha na Francis Godwin)
………………………………………………………………………………..
Na Francis Godwin blog, Iringa
MREMBO
Martha John kuuwakilisha mkoa wa Iringa katika mashindano ya Redds
Miss kanda ya nyanda za juu kusini baada ya kufanikiwa kutwaa taji la
Redds Miss Iringa 2014 baada ya kuwashinda washiriki wenzake nane
waliojitosa katika kinyang’anyiro hicho .
Martha
alitawazwa kuwa mrembo wa mkoa wa Iringa jana usiku katika ukumbi
wa St Dominic shindano lililoshuhudia na kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa
Gerald Guninita .
Kutokana
na ushindi huo Martha kwa sasa ndie atakayeuwakilisha mkoa wa
Iringa katika shindano la kumsaka Redds Miss Kanda ya nyanda za juu
,onyesho linalotarajia kufanyika ijumaa ya wiki ijayo mjini Iringa.
Jaji
mkuu wa shindano hilo Dosi Magambo mbali ya kumtangaza Martha kuwa
mshindi wa kwanza katika kinyang’anyiro hicho pia alimtangaza
mshindi wa pili kuwa ni Elizabeth Titus na mshindi wa tatu ni Fowe
Mkuchu
Akikabidhi
zawadi kwa washindi hao kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa Bw Guninita
alisema kuwa ni imani yake na ya serikali ya Rais Dr Jakaya Kikwete
kuona wasanii na washiriki wa michezo mbali mbali wanaendelea
kufanya vema katika nafasi zao ili kuiwezesha nchi kupiga hatua
katika sanaa mbali mbali.
Post a Comment