Meya
Wa Manispaa ya Ilala Mh Jery Silaa Wa Kwanza kulia akifika eneo la
Tabata St Marrys kukagua kipande cha barabara huyo ambacho kimezua
mgogoro baina na Manispaa na Shirika la maji safi na salama DAWASA.
Mwenyekiti
wa Serikali za Mitaaa Bwana Hassan Chambuso akimuongoza Mh Meya wa
manispaa ya Ilala Jery Silaa kwenda kujionea eneo la kipande cha
barabara ya St Marys Tabata ambacho kinaleta shida baina ya Mkandarasi
na Dawasa
Mkandarasi
wa barabara ya Tabata-St Mary Bwana George Lupia wa pili kutoka
kushoto akitoa ufafanuzi kwa Meya Wa Ilala Mh Jery Silaa kuhusu kukwama
kwake kuendelea na Ujenzi kutokana na Mabomba ya Dawasa kupita Katikati
ya barabara Hiyo.
Meya
wa Ilala Mh Jery Silaa akifafanua Jambo kwa Mwenyekiti wa mitaa ya
Tabata Bwana Chambuso kuhusu yeye Kulifuatilia Swala hilo kwenye mamlaka
husika haraka iwezekanavyo,Pembeni yake ni Diwani wa Kata ya Tabata St
Marys Bi Mtumwa Mohamed mwenye Dira.
Mkandarasi
Geoge Lupia Akimwelezea Meya wa Ilala Mh Jery Silaa kwamba wametumia
pesa nyingi katika kuchimba eneo hilo na kupata usawa wa Barabara lakini
kikwazo kimekuja baada ya kukuta mabomba ya Dawasa ambayo yamekatiza
katikati ya barabara na pembeni Hivyo kuleta ugumu katika kufanikisha
Umaliziaji wake.
Mkandarasi
wa Manispaaa ya Ilala Bwana Kassim Muhinda Akimwelezea Meya Jerry Silaa
kwamba washaongea na Dawasa lakini hawapewi ushirikiano wa kutosha na
wa haraka katika kushughulikia utoaji wa Mabomba hayo
Mkandarasi wa Manispaaa ya Ilala Bwana Kassim Muhinda akiendelea kufafanua jambo kwa Mh Meya wa Ilala Jerry Silaa
Meya wa Ilala Mh Jerry Silaa Akiongea na vyombo vya habari kutoa ufafanuzi wa nini kitafanyika ili kutatua mgogoro huo.
Diwani
wa Kata ya Tabata -St Mary Bi Mtumwa Mohammed Akielezea ni jinsi gani
wanainchi wa eneo hilo wanapata tabu baada ya barabara hiyo kuchimbwa
hivyo kufanya upitaji wa magari kusitishwa kwa mda eneo hilo
Mkandarasi
wa barabara ya Tabata_St Marys Bwana George Lupia akiongea na vyombo
vya habari kuelezea ni ugumu gani anakumbana nao katika utekelezaji wa
ujenzi wa barabara hiyo,kutokana na mabomba ya Dawasco kupita katikati
ya barabara Hiyo
Hiki
ndio kipande cha barabara ya Tabata-St Marys ambacho kinashindwa
kuendelea na matengenezo kutokana na Mabomba ya Dawasa kupita kati kati
ya barabara na pembezoni,hivyo kumpa hali ngumu mkandarasi kuchimba eneo
hilo ili ajaze kifusi.
Pembenini
maji yaliyotuama baada ya Bomba la Dawasa kupasuka Hivyo kuleta
usumbufu kwa mkandarasi kukamilisha ujenzi wa eneo hilo.
Hilo shimo hapo ni bomba amabalo limepita katikati ya barabara
Mmiliki
wa gari hii ndogo Toyota Premio alipatwa na hasira baada ya Gari yake
kushindwa kupanda ili atokee upande wa pili ikambidi kushuka
Kwa hasira mmiliki huyu akatoa vizuizi ya Barabara hiyo na kuvitupa pembeni
Hapo mmiliki huyo akikagua gari yake kama imepata mikwaruzo
Wakiendelea kutazama gari yao kwa umakini
Akaamua kupanda kwa kasi baaada ya vizuizi kutolewa na yeye mwenyewe.
Meya
wa Manispaaa ya Ilala Mh Jerry Silaa ametembelea eneo la Tabata-St Marys
kujionea maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo na pia kuweza kuona
mabomba ambayo yanaleta mgogoro baina ya mkandarasi na Manispaaa na
Dawasa,Akiwa eneo hilo la St Marys Mh Jerry Silaa ameweza kujionea namna
mabomba ya Dawasa ambavyo yamepita katikati ya barabara na pembezoni
yakiwa katika kima kifupi hivyo kumzuia mkandarasi kuendelea na ujenzi
wake.
Akiongea
na vyombo vya habari Mh Meya Amesema kuwa barabara hiyo imetumia
gharama za takribani bilioni 1 lakini imeshindwa kumalizika kwa wakati
kwa sababu ndogo ya Dawasa kutokushirikiana nao ili kuweza kumpa
mkandarasi ramani kamili ya bara bara hiyo,Meya Silaa akaongeza kuwa
wameshawasiliana na wenzao wa Dawasa kuhusu tatizo hilo lakina wamekuwa
hawapewi majibu kwa wakati na ya kuridhisha.Naye mkandarasi wa eneo hilo
Bwana George Lupia amesema kuwa alipewa ramani na manispaa ambayo
haikuonysha kama kuna mabomba ambayo yamepita hapo,lakini wakati ameanza
kuchimba barabara hiyo ndio akakutana na mabomba hayo,Mkandarasi huyo
akaongezea kwamba alishawasiliana na Dawasa kitambo sana lakini hapewi
majibu ya kuridhisha kuhusu kushirikiana nao kuhamisha bomba hizo.
Naye
Diwani wa kata Hiyo Bibi Mtumwa Mohhamed amesema wanainchi wa eneo hilo
wanapata tabu sana kwa kuwa magari yao hayawezi kutoka ndani wala
kuingia kwa kuwa barabara imechimbwa kwa kina kirefu sana,hivyo
amewaahidi wanainchi wa eneo Hilo kwamba wanaendelea kulitatua tatizo
hilo na wenzao wa dawasco ili kuweza kuhamisha mabomba ya eneo hilo. PICHA NA HABARI NA DJ SEK BLOG
Post a Comment