Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ambae ni mtoto wa Rais wa
Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete anasema
‘kuwa mtoto wa Rais changamoto kubwa ambayo nimeiona mojawapo ni watu
kukupa tafsiri ya vitu vingine ambavyo wewe huvijui, kumekua na
malalamiko mengi sana kwamba huyu jamaa ana mali hizi na hizi’
‘Wanasema kampuni za mafuta, Oil Com, Camel Oil na Lake Oil ni za
kwangu, sasa unajiuliza huyo mtu ambae anaweza akatengeneza kampuni tatu
zinazofanya shughuli moja kwa nini asianzishe kampuni moja ikawa kubwa
zaidi ?? kwa hiyo kumekua na manenomaneno mengi, hizo ni changamoto
mfano kwenye siasa huku, watu wengi aidha hawajui nimetokea wapi au
wanajitoa akili katika maana kwamba hawataki kujua nimetoka wapi’
‘Kuna
kipindi unaweza ukashangaa Mwandishi wa habari anachukua kalamu
anaandika maneno mpaka unashangaa kayatolea wapi? sitaki kuamini kwamba
Mwandishi unaweza kuandika kwamba Ridhiwani kapata UNEC kwa sababu ya
baba yake, ungechukua muda ukamsoma Ridhiwani vizuri ukauliza watu
waliokaa na Ridhiwani, uliza huyu ameshawahi kuwa kiongozi??’
‘Wako watu ambao kwa kuwa wamemjua Ridhiwani baada ya Jakaya Kikwete
kuingia Ikulu basi nao wanaanzia hapohapo Ikulu lakini hawajui Ridhiwani
kabla ya baba yake hajawa Ikulu alikua anaishije, mimi nimekua naishi
maisha ya kawaida nimekaa boarding school nimesoma Mkwawa baba yangu
akiwa Waziri, nilikua na uwezo wa kwenda kusoma Ulaya lakini nimesoma
chuo kikuu Dar es salaam pale japo nilikua na uwezo wa kwenda popote
pale ninapotaka ila ni kwa sababu tu mzee wangu alitaka kuona naishi
kama watu wengine’
Post a Comment