UONGOZI wa serikali mkoani hapa, umesema hakuna ajali iliyotokea
ikihusisha msafara wa Mkuu wa Mkoa, Said Magalula na kumjeruhi Katibu
Tawala wa Mkoa, Severine Kaitwa.
Akizungumza na Mwandishi wa habari hii kwa njia ya simu,
Mkuu wa Wilaya (DC) ya Geita, Omar Mangochie, alisema taarifa
zilizochapishwa katika gazeti la Tanzania Daima Jumatano, toleo la Juni 15 hazikuwa sahihi.
Mangochie alisema licha ya kutokuwepo kwa ajali, hata mkuu wa mkoa yupo China tangu Juni 9, mwaka huu.
“Hii habari imetushangaza na kutuletea matatizo maana viongozi wetu
wote wapo salama na hakuna msafara wala ajali iliyotokea kama
mlivyoandika.
“Inaonekana aliyetunga uongo huu na kuutuma kwenu ana nia ovu kwa viongozi wa serikali,” alisema Mangochie.
Post a Comment