********
Dar es Salaam. Makamu Mwenyekiti mstaafu wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Pius Msekwa ametoboa siri ya chama hicho
kung’ang’ania Muungano serikali mbili akisema hiyo ndiyo sera yake pekee
iliyopitishwa na wanachama wake wote kwa kura ya maoni.
Msekwa alieleza hayo katika mahojiano maalumu na wahariri wa gazeti hili yaliyofanyika nyumbani kwake Oysterbay, Dar es Salaam.
Msekwa ambaye katika habari iliyochapishwa na
gazeti hili jana alieleza kuwa binafsi, hana tatizo na suala la idadi ya
Serikali katika Muungano, alisema kamwe hawezi kukishauri chama chake
kukubaliana na mapendekezo ya Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya
Mabadiliko ya Katiba ya muundo wa serikali tatu.
“Siwezi kuishauri CCM kukubali serikali tatu. Hili
la Serikali mbili ni sera ya CCM, siyo tu sera ya kawaida, bali hii ni
sera pekee iliyopitishwa na wanachama wote kwa kura ya maoni,” alisema
Msekwa ambaye pia ni Spika mstaafu wa Bunge.
Alisema tofauti na sera hiyo ya serikali mbili,
sera nyingine za chama hicho huanzia katika ngazi ya Kamati Kuu,
kujadiliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) na kupitishwa na Mkutano
Mkuu wa Taifa.
Msimamo ulikoanzia
Kiini cha sera hiyo kutengenezewa utaratibu
maalumu, kilitokana na sakata la Kundi la Wabunge 55 (G55), kuanzisha
agenda ya kutaka Serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano na hatimaye
Bunge kupitisha Azimio la kuanzisha serikali hiyo.
Msekwa ambaye wakati huo alikuwa Naibu Spika
lakini akiongoza Bunge kutokana na aliyekuwa Spika, Chifu Adam Sapi
Mkwawa kuwa mgonjwa, alisema ushauri wa kurudi kwa wanachama wa CCM
kuwauliza wanataka serikali ngapi ulitolewa na Mwalimu Julius Nyerere.
Itakumbukwa kuwa hatua ya Bunge kupitisha azimio
hilo la kuanzisha Serikali ya Tanganyika ilimkera Mwalimu hadi akatunga
kitabu, Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania akiwashutumu aliyekuwa Waziri
Mkuu, John Malecela na aliyekuwa Katibu Mkuu wa (CCM), Horace Kolimba.
“Mwalimu alitueleza kwenye Halmashauri Kuu ya Taifa, kuwa Bunge
limekwishapitisha azimio na likipitishwa ni lazima litekelezwe na
Serikali. Alisema mkikataa azimio la Bunge hivihivi mtaleta mgongano wa
kikatiba, msiamue peke yenu, nendeni kwa wanachama wote muwaulize ili
uamuzi uwe wa wote,” alisema.
Alisema kutokana na ushauri huo, mwaka 1993 CCM
iliandaa na kusimamia upigaji kura za siri za maoni katika kila tawi,
wanachama wakitakiwa kujadili na kuchagua kati ya serikali moja, mbili
au tatu.
“Matokeo yalipofika katika Halmashauri Kuu,
ilionekana wanachama walio wengi katika matawi mengi walitaka serikali
mbili, na hapo ndipo ikapitishwa sera ya serikali mbili,” alisema na
kusisitiza:
Post a Comment