TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 20.06.2014.
- MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI AUAWA KWA KUPIGWA JIWE KICHWANI.
- MFANYABIASHARA MMOJA MKAZI WA CHANG’OMBE WAILAYANI CHUNYA AVAMIWA NA KUPORWA VITU MBALIMBALI.
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA TUHUMA TOFAUTI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MWANAFUNZI
WA KIDATO CHA PILI KATIKA SHULE YA SEKONDARI NZONDAHAKI ALIYETAMBULIKA
KWA JINA LA JOSHUA BUKUKU (19) MKAZI WA NZOVWE AMEUAWA KWA KUPIGWA JIWE
KICHWANI NA MTU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JOSHUA SAID (17) MKAZI WA
SIMIKE.
INADAIWA
KUWA MNAMO TAREHE 18.06.2014 MAJIRA YA SAA 17:00 JIONI HUKO KATIKA
UWANJA WA SHULE YA SEKONDARI ST.MARTS ILIYOKO ENEO LA FOREST MPYA, KATA
YA FOREST, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA ULITOKEA UGOMVI BAINA
YA MAREHEMU NA MTUHUMIWA WAKATI WAKICHEZA MPIRA WA MIGUU NA NDIPO
MTUHUMIWA KUMPIGA JIWE LA KICHWANI NA KUMJERUHI.
MHANGA
ALIFARIKI DUNIA MNAMO TAREHE 19.06.2014 MAJIRA YA SAA 18:32 JIONI
WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
INADAIWA KUWA MTUHUMIWA ALIKUWA ANASOMA SHULE MOJA NA MAREHEMU NA
ALIACHA MASOMO AKIWA KIDATO CHA TATU MWAKA 2013. MTUHUMIWA AMEKAMATWA.
MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MFANYABIASHARA
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA STEVEN DAISON (33) MKAZI WA CHANG’OMBE
ALIVAMIWA AKIWA NYUMBANI KWAKE NA WATU WANNE ANAOWAFAHAMU KWA SURA NA
KUMJERUHI KWA KUMKATA MAPANGA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA KISHA
KUPORA VITU MBALIMBALI.
TUKIO
HILO LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 01:00 USIKU KATIKA
KITONGOJI CHA MWAGALA, KIJIJI CHA CHANG’OMBE, KATA YA MBUYUNI, TARAFA YA
SONGWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA HAO WALIMJERUHI
MHANGA KWA KUMKATA MAPANGA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA KISHA
KUMPORA PESA TSHS 1,800,000/=, SIMU PAMOJA NA VOCHA ZA SIMU ZENYE
THAMANI YA TSHS1,200,000/=.
INADAIWA
KUWA, KABLA YA TUKIO WATU HAO WALIFYATUA RISASI HEWANI NA GANDA MOJA LA
RISASI YA S/GUN LIMEOKOTWA ENEO LA TUKIO. MHANGA AMEPATIWA MATIBABU NA
KURUHUSIWA. MSAKO MKALI UNAENDELEA ILI KUWABAINI WATUHUMIWA WA TUKIO
HILI.
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL
MASAKI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI WALIPO WATUHUMIWA
WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA
KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
TAARIFA ZA MSAKO:
KATIKA MSAKO WA KWANZA:
MTU
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA LAITON ANYELWISYE (32) MKAZI WA KIJIJI
CHA UPENDO ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE
HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 5.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 19.06.2014 MAJIRA YA SAA 09:00 ASUBUHI KATIKA
KIJIJI CHA UPENDO, KATA YA MAMBA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA
CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
MSAKO WA PILI:
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA RAIA NA MKAZI WA NCHINI
ETHIOPIA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA KADIL KANDAM (22) AKIWA AMEINGIA
NCHINI BILA KIBALI.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 19.06.2014 MAJIRA YA SAA 23:00 USIKU KATIKA
ENEO LA IGAWILO, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA
MBEYA.
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL
MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARMU YA MOSHI [GONGO]
KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA
ANATOA WITO KWA WANANCHI KUENDELEA KUTOA TAARIFA ZA WATU WANAOWATILIA
MASHAKA KATIKA MAENEO YAO HASA WAHAMIAJI HARAMU ILI UPELELEZI UFANYWE
DHIDI YAO.
[BARAKAEL MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment