Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MZUNGU ALIYEDAIWA KUTUPA MKATE MANISPAA YA MOSHI AZUA MAKUBWA KWA ASKARI, TAZAMA PICHA HIZI

 


Baada ya kuzunguka kwa muda mrefu raia huyu wa kigeni ambaye haikufahamika mara moja anatoka nchi gani aliketi katika kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi kisha akatoa Mkate huku akiulainisha na Jam na kuanza kula.Alikula Silesi kadhaa lakini alionekana mwingi wa mawazo kila alipotafuna mkate.  
Baadae akasukumia mkate na Maji ya Kilimanjaro.Akafunga maji yake akayarudisha ndani ya begi lake.Akaendelea kutafuna Mkate.Akamuuliza mtu aliyekuwa jirani yake vipi unahitaji na wewe nikupatie kidogo na hii ilikuwa ni silesi ya mwisho.
Baada ya kupita muda mgeni huyo aliamua kuondoka eneo alilokuwa ameketi akipata mkate wake wa kila siku.Ghafla nyuma yake akajitokeza askari wa manispaa ya Moshi (Mwenye t-shirt nyeupe) ambaye ana jukumu la kusimamia maswala ya mazingira. 
Baada ya kufuatilia kwa kina ,ikagundulika kuwa askari huyo alikuwa anamfuatilia mgeni huyo akitaka kumtia mikononi kwa kosa la kutupa taka ambazo ni vipande vya mikate na kopo la Jam na kama unavyofahamu sheria za usafi kwa manispaa yetu ya Moshi. 
Globu ya jamii ikabahatika kuona vipande vya mikate lakini ilipomuuliza askari huyo ni vipi mbona hajamkamata na kumpeleka kunako husika kama wafanyavyo kwa wabongo wenzao ,askari huyo ambaye jina lake halikufahamika mara moja alisema anataka kumkamata lakini hawaelewani lugha huku akidai kuwa yeye kimombo hakipandi akalazimika kwenda kuomba msaada kwa asakri polisi kata aliyekuwa katika kituo hicho cha mabasi. 
Raia huyo wa kigeni akaondoka zake.Kumbe askari yule wa mazingira aliyeenda kuomba msaada kwa askari polisi aliyekuwa katika kituo hicho cha mabasi alikutana na zahama nyingine wakati akiomba msaada kwa asakari huyu anayeonekana hapa ya kupigwa makofi kwa madai aligoma kwenda kutoa msaada wa kumkamata yule raia wa kigeni kwa kuwa haujui "Kizungu",na hapa asakari huyo aliamua kumueleza mwenzake (mwenye t-shirt nyeupe)aliyetambulika kwa jina la Mkude kuhusu tukio hilo ndipo Mkude kwa ghadhabu ya hali ya juu akaenda kuwakamata asakari hao wa mazingira. 
Wakati asakari hao wa mazingira wakifanya utaratibu wa kumakamata raia huyo wa kigeni ghafla walidakwa na Mkude wote wawili. 
Kisha safari ya kwenda Kituoni ikaanza.
Wakati asakari hao wa mazingira wakifanya utaratibu wa kumakamata raia huyo wa kigeni ghafla walidakwa na Mkude wote wawili .
Kisha safari ya kwenda Kituoni ikaanza.
Ghafla Mkude baada ya kuona kamera ya globu ya jamii inammulika alimuamuru askari mwenzake kuikamata ,alakini hata hivyo askari yule alifahamu kuwa Globu ya jamii pia iko kazini kama walivyo wao.
Mzobe mzobe ukaendelea kupita katikati ya kituo kikuu cha mabasi huku mbinje za kutosha toka kwa wakatisha tiketi na wapiga debe zikirindima.
Askari Polisi.Mkude akafanikiwa kuwatia mikononi askari wa manispaa ya Moshi wanaoshughulika na mazingira hadi kituoni.Globu ya jamii ilifika hadi kituoni licha ya kwamba asakri wa kata aliyekuwa amevalia sare kudai kuwa yeye aliwasamehe lakini Mkude akiwa kituoni alisimamia msimamo wa kufunguliwa kwa kesi dhidi ya sakari hao.Hata hivyo baadae raia wa kigeni alionekana katika eneo la stendi akiranda randa.
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top