Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
KAMATI
ya uchaguzi ya klabu ya Simba inatarajia kuanika orodha ya mwisho ya
wagombea wa nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa klabu hiyo unaotarajia
kufanyika juni 29 mwaka huu jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti
wa kamati hiyo, wakili Dkt. Damas Daniel Ndumbaro amesema kamati yake
ilikuwa na kikao leo hii kwa ajili ya kufanya maandalizi ya kuelekea
ukingoni mwa shughuli nzima ya uchaguzi.
“Kesho
kunako saa 5:00 asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa TFF tutakuwa na
mkutano na waandishi wa habari kuwaeleza mambo mengine pamoja na orodha
ya mwisho ya wagombea, orodha ya wale ambao wamevuka vikwazo na
watashiriki uchaguzi wa Simba sc”. Alisema Ndumbaro.
Aidha
Dkt. Ndumbaro aliongeza kuwa baada ya kutangaza orodha hiyo ya mwisho,
kamati yake itatoa ruksa ya wagombea kuanza kampeni rasmi kwa wanachama
wa klabu ya Simba.
“Kwasababu
kanuni inasema angalau siku tano, tukishawatangaza kesho, wataweza
kuingia msituni na kuanza kazi ya kunadi sera zao”. Alisema Ndumbaro.
Hata
hivyo, Dkt. Ndumbaro alisisitiza kuwa kampeni ziwe za utulivu,
ustaraabu na zisiwe za lugha ya matusi, bali wagombea wauze sera zao ili
wanachama waweze kuamua nani anafaa kwa manufaa ya klabu ya Simba.
Post a Comment