Mnenguaji
wa Kundi la Kanga Moko, Zawia Hamis ambaye usiku wa Jumatano iliyopita
alipigwa risasi mbili mwilini na mtu aliyedaiwa ni askari polisi,
ameweka undani wa sakata hilo.
Akizungumza
na Risasi Jumamosi juzi nyumbani kwake Mwananyamala jijini Dar,
majeruhi huyo alisema tukio hilo lilijiri maeneo ya Mwananyamala-
Kisiwani karibu na Ofisi za Chama cha Wananchi (Cuf) na kuongeza kuwa,
kisa ni kubishana na askari huyo aliyetaka kuzimwa kwa matarumbeta
kutoka kwenye kikundi chao kilichokuwa kikipita eneo hilo.
“Sisi
tulikuwa tukipita na matarumbeta, askari wakatusimamisha na kutuamuru
tuyazime kisha kutaka kutukamata watupeleke kituoni eti serikali
imekataza.
“Tuliwaambia
mbona ni mapema sana kwani ilikuwa saa kumi alasiri na Kova alisema
ngoma za Kanga Moko, Kigodoro na nyingine zisipigwe usiku. Pia
tuliwaambia tulichokuwa tukikifanya si ngoma hasa, ni matarumbeta
tunapita kuwaalika watu kuwa leo kuna shughuli sehemu.
“Baada
ya majibu hayo ndipo askari mmoja hakutaka hata kuendelea na
mazungumzo, alitoa bastola kiunoni na kunipiga risasi mbili, moja
kiunoni, nyingine kwenye mbavu halafu akapiga tena hovyo hewani risasi
zilizobaki. Kwa kweli nimeumia sana,” alisema Zawia.
Mnenguaji
huyo alisema kutokana na hali yake kuwa mbaya alipelekwa Kituo cha
Polisi cha Mwinjuma na kupewa Polisi Fomu No. 3 (PF3) kisha kukimbizwa
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kinondoni, Mwananyamala kwa ajili ya
matibabu ambapo kwa mujibu wake alitolewa risasi mbili.
Baada ya kuzungumza na majeruhi huyo, waandishi wetu walikwenda kwenye Kituo cha Polisi Mwinjuma ambako ndiko alikoripoti PF3.
Baada ya kuzungumza na majeruhi huyo, waandishi wetu walikwenda kwenye Kituo cha Polisi Mwinjuma ambako ndiko alikoripoti PF3.
Askari
mmoja wa kituo hicho (jina lipo) alisema hawezi kusema lolote kuhusu
tukio huku akiweka wazi kwamba, afande aliyempiga risasi mnenguaji huyo
anajulikana hivyo mlalamikaji anaweza kwenda mbele ya sheria.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Dar, Camillius Wambura hakupatikana kwa simu juzi kuzungumzia tukio hilo.
Post a Comment