THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
|
PRESIDENT’S
OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O.
BOX 9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametaja
misingi mikuu mitano ambayo utekelekezaji wake unathibitisha kushamiri kwa
utawala bora nchini.
Aidha,
Rais Kikwete amesema kuwa pamoja na kwamba utawala bora unaendelea kushamiri
nchini, bado taasisi za usimamizi wa masuala ya utawala bora zina nafasi ya
kuboresha kazi yao na kupanua kwa kiasi kikubwa zaidi utawala bora.
Rais
Kikwete aliyasema hayo usiku wa jana, Jumatatu, Juni 23, 2014, wakati
alipozungumza baada ya kuwa ametunukiwa Tuzo ya Kutambua Mchango Wake wa
Kuimarisha Utawala Bora nchini ambayo imetolewa na taasisi nane za usimamizi
nchini.
Taasisi
hizo ni Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa
Hesabu (NBAA), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCB), Mamlaka ya
Manunuzi ya Umma (PPRA), Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Jamii (SSRA), Ofisi
ya Mhasibu Mkuu wa Serikali (ACCGen-D), Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali
(IAG-D) na Sekretarieti ya Tume ya Maadili.
Hiyo
ni mara ya kwanza kwa Tuzo hiyo kutolewa nchini na ilikabidhiwa kwa Rais
Kikwete wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa kwa ajili ya wajumbe wa
Mkutano wa Mwaka wa Wakaguzi wa Hesabu za Serikali kwenye Ukumbi wa Mikutano wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) mjini Dar Es salaam.
Mkutano
huo wa mwaka pia unahudhuriwa na wajumbe waalikwa kutoka nchi za Ujerumani,
Afrika Kusini, Uganda, Sweden, Sierra Leone, Nigeria, Niger, Ghana, Kenya,
Zambia, Rwanda, Burundi na Ethiopia. Akizungumza
baada ya kukabidhiwa Tuzo hiyo na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG) Bwana Ludovick Utoh, Rais Kikwete alisema kuwa Tanzania ina
utawala bora kwa sababu inadumisha misingi yote mikuu ya utawala bora.
Aliitaja
misingi hiyo kuwa ni kushamiri wa demokrasia, uhuru wa kutoa maoni na wa vyombo
vya habari, haki ya kila Mtanzania kuishi, utawala wa sheria, kutoingiliana kwa
mihimili mitatu ya Serikali.
Rais
Kikwete ambaye amesema kuwa amepokea Tuzo hiyo kwa niaba ya viongozi wenzake
katika Serikali – Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Katibu
Mkuu Kiongozi, Makatibu Wakuu na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama –
amesema kuwa utawala bora ni jambo muhimu na halina mbadala wake.
“Tanzania
tumeruhusu uhuru mkubwa kwa wananchi wetu kushiriki katika shughuli zao.
Serikali yetu haitishi watu wake. Hatufanyi hivyo. Ziko nchi zinaishi kwa
kutisha raia wake na nyie mnazijua, “
alisema Rais Kikwete.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM
24 Juni, 2014
Post a Comment