Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amesema kuwa mfumo wa vyama vingi vya siasa ni mzuri, umeleta matumaini
kwa kupanua wigo na kufungua zaidi uwanja wa kisiasa pamoja na
kuiwajibisha Serikali.
Hata
hivyo, Rais Kikwete amesema kuwa ili mfumo huo uboreshwe zaidi na uweze
kuimarisha misingi mikuu ya maendeleo ni lazima uendeshwa kwa watu
kufuata sheria na wala siyo kuingiza matumizi ya nguvu ambayo yanaweza
kuvuruga nchi.
Rais
Kikwete ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama
aliyasema hayo jana, Ijumaa, Juni 20, 2014, wakati alipotoa Mhadhara
(Lecture) kuhusu Usalama wa taifa – The Security of a Nation- kwenye
Chuo cha Taifa cha Ulinzi - National Defence College (NDC) Kunduchi,
mjini Dar Es Salaam.
Rais
Kikwete alikuwa anajibu swali la mwanafunzi wa kozi ya pili kwenye chuo
hicho kutoka Kenya ambaye alitaka kujua jinsi gani vyama vingi vya
siasa vinavyoathiri umoja wa kitaifa na kuibadilishaTanzania kufuatia
miaka zaidi ya 30 ya Tanzania kuwa nchi yenye kuleta matumaini kwa nchi
nyingine za Afrika na Waafrika.
Rais
kikwete alisema: “Vyama vingi ni vizuri. Mfumo wa vyama vingi unaleta
matumaini kwa kupanua wigo wa kisiasa ambao haukuwa mpana kiasi hicho
huko nyuma. Sasa mtu anaweza kuamua kujiunga na chama chochote cha siasa
anachokipenda yeye.”
Aliongeza
rais Kikwete: “Ni mfumo ambao unaiwajibisha Serikali. Ni mfumo mzuri
kwa upanuzi wa demokrasia. Sasa watu wanaweza hata kuamua kupunguza
bajeti ya safari za Rais nje ya nchi. Wanadhani kuwa Rais anaweza
kufanikiwa zaidi na Tanzania kupita hatua za maendeleo haraka zaidi kama
Rais atabakia amejifungia ndani ya nchi.”
Rais
Kikwete alizidi kujibu swali hilo: “Jambo la maana ni kwamba tunahitaji
aina mbali mbali ya mawazo. Mawazo ya namna hiyo hayaathiri demokrasia.
Mawazo ya namna hiyo yanasaidia hata chama changu kuimarika zaidi.”
Hata
hivyo, Rais Kikwete amesema kuwa mfumo huo utavurugika endapo baadhi ya
watu wataendekeza matumizi ya nguvu na hoja za nguvu badala ya
kupambana kwa hoja na nguvu ya hoja.
“Wasiwasi
wangu ni kuingiza matumizi ya nguvu katika ujenzi wa demokrasia. Ni
makosa kwa watu kukimbilia kutumia nguvu baada ya kushindwa kwenye hoja.
Na hili halivumiliki na likitokea basi Serikali itaingilia kati
kudumisha amani.”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM
21 Juni, 2014
Post a Comment