Serikali
imempa wiki tatu mkandarasi anayetengeneza barabara ya kilomita tatu ya
kuingia makao makuu ya wilaya ya Lushoto kuwa awe amekamilisha kazi
hiyo baada ya kupewa asilimia 90% ya fedha za ujenzi wa barabara hiyo
kwa kiwango cha lami la sivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi
yake.
Akizungumza
na ITV ofisini kwake kuhusu miradi ya barabara katika wilaya hiyo
inavyozorota huku serikali ikiendelea kutoa fedha kwa baadhi ya
wakandarasi lakini barabara hizo hazina tija, mkurugenzi wa
halmashauriya wilaya ya Lushoto Bwana Jumanne Shauri amesema hadi sasa
mkandarasi huyo amekwisha pewa fedha kiasi cha shilingi milioni 240 kati
ya shilingi milioni 390 za mradi huo lakini ujenzi huo umechukua zaidi
ya mwaka bado kukamilika.
Katika
hatua nyingine wilaya ya Lushoto imepata tuzo kwa kushika nafasi ya
tatu katika zoezi zima la utunzaji mazingira hatua ambayo imesababisha
uoto wa asili katika wilaya hiyo kuanza kurejea baada ya kuanza
operesheni ya kupanda miti kuanzia shuleni hadi majumbani kufuatia
baadhi ya watu kwa kushirikiana na baadhi ya wafanyabiashara kuharibu
vibaya misitu ya asili ya hifadhi katika kipindi cha miaka minne
iliyopita.
Baadhi
ya watendaji wa halmashauri hiyo waliojikita na mazingira wamesema hivi
sasa wanafanya operesheni ya kuwakamata na kuwafikisha katika mabaraza
ya kata baadhi ya wakazi ambao hawana vyoo ili kuhakikisha wanaimarisha
usafi wa mazingira katika maeneo tofaut wilayani Lushoto.
Post a Comment