Wafanyakazi
wa Shirika la Madini la Taifa STAMICO wakiwahudumia wageni
waliotembelea katika banda lao kwenye maonyesho ya wiki ya Utumishi
yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam. Wafanyakazi
wa Shirika la Madini la Taifa wakiangali moja ya majarida ya nayoelezea
shughuli za shirika hilo kutoka kulshoto ni Bibiana Ndumbaro, Denis
Silas na Charles Mawala. Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Shirika la Madini la Taifa STAMICO Bw.
Leornald Mwakalebela akiwapatia majarida wafanyakazi wenzake ili
kuwagawia wananchi wanaotembelea banda hilo.
Wafanyakazi wa Shirika la Madini la Taifa wakiwa katika picha ya pamoja kwenye banda lao.
....................................................................................
Na Mwandishi Wetu
KAIMU
Mkurungenzi Mtendaji mpya wa Shirika la Madini la Taifa, Mhandisi Edwin
Ngoyani ameahidi neema kwa wachimbaji wadogo wa madini na vito nchini
kwa kuwawezesha kupata masoko ya bidhaa zao pamoja na kuwapatia zana za
kisasa za uchimbaji madini.
"Malengo
yangu makuu katika shirika hili ni kuhakikisha wachimbaji wadogo
wanawezeshwa kunufaika na rasilimali za nchi yetu pamoja na kuhakikisha
kwamba STAMICO linatoa mchango wa mapato katika mfuko mkuu wa hazina kwa
kujiendesha kwa faida," Mhandisi Ngonyani alisema katika mkutano na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
kwa kujiamini, Mhandisi Ngonyani alisema anatarajiwa malengo yake
katika STAMICO yataanza kuzaa matunda ndani ya miaka miwili mpaka mitatu
ijayo.
Akizungumzia
mkakati kwa wachimbaji wadogo, Ngonyani alisema,ndani ya miaka miwili
ijayo, shirika hilo litanunua mitambo miwili ya uchimbaji wa madini ya
kisasa (drilling rigs) ambayo itatumiwa na wachimbaji wadogo.
“Lengo
ni kuwafanya wachimbaji wadogo wanufaike na wawe sehemu ya uwekezaji
kwenye rasilimali zao, kama ambavyo hao wawekezaji wa nje wanavyowekeza,
na sasa watanzania nao watawekeza, ila lazima tuwawezeshe," Ngonyani
alisisitiza.
Alisema
lengo la STAMICO kwa wachimbaji wadogo ni kuhakikisha wanawezeshwa
kuwekeza na kuchimba kisasa ili pia watoa mitaji ambao ni benki wawe na
uhakika wa fedha zao kurejeshwa, na kwamba hata ikibidi, shirika hilo
litawawekea dhamana ili wawezeshwe kibenki.
Alisema
hilo litawezekana baada ya mkakati wao wa kuanzisha na kuboresha
takwimu za wachimbaji wadogo ambazo zitakuwa na taarifa zao ikiainisha
mahali walipo,aina ya madini wanayochimba na mahitaji yao.
Pia
mkakati mwingine ni kubaini vyanzo vya migogoro kwenye maeneo ya
wachimbaji na kutafuta suluhu ikiwa ni pamoja na kutenga maeneo
yanayofaa kwa uchimbaji mdogo ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima. Katika
hatua nyingine, Ngonyani alizungumzia mradi wa uchimbaji madini kwenye
mgodi dhahabu wa Tulawaka ambao hivi sasa umenunuliwa na shirika hilo na
kuitwa Biharamulo unaosimaimamiwa na kampuni ya StamiGold.
Alifafanua
kwamba mgodi huo utaanza kazi rasmi Agosti 8, mwaka huu na kwamba baada
ya miaka miwili na nusu, wanatarajia kupata faida ya shilingi bilioni
saba. Awali mgodi huo ulikuwa ukimilikiwa na kampuni ya
African Barrick Gold (ABG) na mwishoni mwa mwaka jana STAMICO ikaununua
kwa dola za Marekani milioni tano.
ABG
iliuza mgodi huo kutokana na kwamba kiasi cha wakia 100,000 kilichopo
katika eneo la mradi ni kidogo kwa uchimbaji mkubwa kwa kampuni hiyo
kubwa ya madini duniani.
"Hata
hivyo tuna matumaini kwamba katika eneo la kilometa nne kutoka kwenye
eneo la mradi kuna uwezekano wa kuwapo mashapo ya kati 150,000 mpaka
200,000. Tutaendelea na utafiti katika eneo hili," Mhandisi Ngonyani
alisema.
Kwa
upande wake, Meneja Uchorongaji wa Stamico, Alex Rutagweleka alisema
hivi sasa miradi mitano iko kwenye ubia na shirika hilo kwa ajili ya
uwekezaji na kuitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na ule wa Itetemia mgodi
wa dhahabu ambao Stamiko wameingia ubia na Kampuni ya Madini ya Tancan
Ltd.
Mradi
mwingine ni wa Buckreef wa dhahabu ulioko Geita ambao Stamico wameingia
ubia na Kampuni tanzu ya TANZAM 2000, ambapo Stamico wana hisa asilimia
45 na 55 iko kwa kampuni hiyo na kwamba wanategemea uzajishaji utaanza
Novemba mwama huu.
Aidha mradi mwingine ni Kiwira ambao unazalisha makaa ya mawe kwa ajili ya kufua umeme utakaounganishwa kwenye gridi ya taifa. Akizungumzia
mradi huo,Meneja fedha na Utawala wa Stamico, Peter Gembe alisema lengo
la mradi huo ni kufua megawati 200 za umeme kwa ajili ya kuunganisha
kwenye gridi ya taifa kutoka kwa kiwango cha awali cha megawati 6.
Stamico
ni shirika la umma lililoanzishwa mwaka 1972 kwa lengo la kuongeza
mchango wa sekta ya madni katika pato la taifa na kuzalisha nafasi za
ajira kwa watanzania.
Post a Comment