Hatua ya Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuandika upya daftari la kudumu la wapiga
kura, imeendelea kupingwa kwamba haijavishirikisha vyama vya siasa
nchini kama wadau muhimu.Katika mahojiano na Tanzania Daima Jumapili,
Katibu Mkuu wa NCCR – Mageuzi, Mosena Nyambabe, alisema NEC itegemee
changamoto nyingi kujitokeza katika mchakato ambao wameupanga na
Serikali ya CCM."NEC haikutakiwa kufundishwa kwamba ikae na wadau katika
mchakato huu. Inajua kabisa kabla ya uchaguzi mkuu wowote wanapaswa
kuboresha daftari kwa kushirikiana na wadau, inakuwaje sasa wameamua
kufanya peke yao?" alihoji Nyambabe.
Alisema
kama wadau wangeshirikishwa jambo hilo wasingekubaliana na NEC kutumia
teknolojia mpya ya Biometric Voter Registration (BVR) kutoa vitambulisho
ambayo alidai imesababisha matatizo mengi katika chaguzi za nchi za
Afrika.
"Nchi za
Afrika kama Ghana, Zambia, Malawi, Afrika Kusini na nyingine nyingi
zimekuwa na ugomvi mkubwa kati ya tume zao za uchaguzi na vyama vya
siasa wakati wa kujumlisha na kutoa matokeo," alisema.
Mhadhiri
wa Chuo Kikuu cha Bukoba, Dk. Azaveli Lwaitama, alihoji ni kwanini
serikali kupitia NEC itoe taarifa hiyo muhimu pasipo kuwashirikisha
wadau ambao ndio wateja wao.
"Sidhani
kama serikali ina nia ya dhati ya kuandikisha upya daftari la kupiga
kura kwa Watanzania. Kama walikuwa nayo, walipaswa kuwashirikisha wadau
kwa ajili ya kupata maoni ili kuondoa kelele nyingi wakati wa uchaguzi,"
alisema.
Dk. Lwaitama alisema kitendo cha NEC kutumia mfumo wa BVR ambao umekuwa ukikosolewa na wadau katika nchi za Afrika ni hatari.
Post a Comment