Mgeni
rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwezeshaji wa Uchumi Dkt.
Mary Nagu akifungua semina ya Wabunge kuhusu Itifaki ya Umoja wa Fedha
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jana katika ukumbi wa Bunge wa Msekwa
mjini Dodoma. Kulia ni Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum.
Waziri
wa Fedha Saada Mkuya Salum akisisitiza umuhimu wa Itifaki ya Umoja wa
Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Wabunge katika semina
iliyofanyika jana ukumbi wa Bunge wa Msekwa mjini Dodoma.
Mkurugenzi
Msaidizi Sekta za Uzalishaji Wizara ya Afika Mashariki Dkt. Abdula
Makame akiwaeleza Wabunge umuhimu wa Itifaki ya Umoja wa Fedha wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa semina iliyofanyika jana katika
ukumbi wa Bunge wa Msekwa mjini Dodoma.
Mkurugenzi
wa Masuala ya Utafiti wa Uchumi na Sera Benki Kuu ya Tanzania Dkt.
Joseph Masawe akitoa mada juu ya Majukumu ya Benki Kuu ya Afrika
Mashariki na Benki Kuu Wanachama na Nchi wanachama walivyojifunza
kutoka Umoja wa Ulaya wakati wa semina ya Wabunge iliyofanyika jana
katika ukumbi wa Bunge wa Msekwa mjini Dodoma.
Mchungaji
Luckson Mwanjale, mbunge wa Mbeya Vijjini akichangia hoja juu ya
Itifaki ya Umoja wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jana mjini
Dodoma.
Sara
Msafiri (Viti Maalum) akichangia mada juu ya itifaki ya Umoja wa Fedha
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa semina ya Wabunge iliyofanyika
jana katika ukumbi wa Bunge wa Msekwa mjini Dodoma.
(Na Mpiga picha wetu)
CHANZO FULL SHANGWE
Post a Comment