WANAWAKE wengi wa Tarafa ya Mwese katika Halmashauri ya Wilaya ya
Mpanda mkoani Katavi, wanalazimika kujifungulia nyumbani kutokana na
kunyimwa huduma kwenye kliniki baada ya kushindwa kwenda na waume
zao kupimwa afya.
Hayo yalielezwa na Diwani wa Viti Maalumu, Thiodela
Kisesa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani, akisema wajawazito wa
tarafa hiyo wamekuwa wakikosa huduma ya kupimwa maendeleo ya afya
zao kliniki kutokana na watoa huduma kuwakatalia wakitaka waende na
waume zao.
Alisema wanaume wengi wamekuwa wakitakiwa kwenda na wake zao kupima
afya ili kubaini mapema kama wameambukizwa virusi vya ukimwi (VVU)
kuzuia vifo vya mama na mtoto.
Kisesa aliongeza kuwa kutokana na sharti hilo ambalo wanaume
wanalikwepa, wajawazito wengi wamejikuta wakilazimika kujifungulia
majumbani, hali ambayo inahatarisha uhai wa mama na mtoto.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Joseph Msemwa, alilieleza Baraza la
Madiwani kuwa jukumu la kupimwa afya sio la mama peke yake, bali wote
wawili na waume zao.
Alisema wapo wanaume wanaodhani kwamba mama akipimwa na kuonekana
hana maambukizi ya VVU basi nao hawana, jambo ambalo alisema sio sahihi
hata kidogo.
NA Walter Mguluchuma
Post a Comment