Watu wanaotazama runinga kwa saa tatu au zaidi kila siku wako katika hatari ya kuaga dunia
mapema kuwaliko wale wanaotazama kwa muda mchache.
Hii ni kwa mujibu wa uchunguzi uliochapishwa katika jarida la the American Heart Association nchini Marekani.
"Utazamaji sana wa wa runinga ni tabia
ya watu wasio na kazi ya kufanyatu na kuna ongezeko la mienendo ya kila
aina ya tabia za kukaa tu," mtafiti mkuu Miguel Martinez-Gonzalez,
profesa wa chuo kikuu cha Navarra iliyoko Pamplona, nchini Uhispania,
alisema katika taarifa ya shirika hilo.
"Matokeo ya utafiti wetu ni sambamba
na utafiti tuliowahi kufanya, ambapo muda unaotumiwa kutazama runinga
uliolinganishwa na idadi ya vifo vinavyotokea kwa sababu hiyo."
Watafiti hao waliwachunguz vijana
wachanga 13,284 kutoka Uhispania wenye afya na waliohitimu chuo kikuu
kuhusu aina tatu ya tabia za kukaa tu na hatari ya kuaga dunia kutokana
na sababu zote:muda wa kutazama runinga, muda wa kutumia tarakilishi na
muda wa kuendesha gari.
'Sababu nyinginezo'
Vijana hao walioshiriki, ambao
walikuwa na umri wa wastani wa miaka 37 na ambao asilimia 67 walikuwa
wanawake, walifuatiliwa kwa takriban miaka 8.2. mwishowe, vifo 97
viliripotiwa, vikiwemo vifo 19 vilivyotokana na mishipa na moyo, 46
kutokana na saratani na mengine 32 vilivyotokana na sababu nyinginezo.
Utafiti huo ulionyesha hatari kubwa ya
kuaga dunia ilikuwa mara mbili zaidi kwa washiriki walioripoti kutazama
runinga kwa saa tatu au zaidi kwa siku ikilinganishwa na wale
waliotazama kwa saa moja au chini ya saa.
Watu 19 waliripotiwa kufariki kutokana na kutizama TV kwa muda mrefu
Hatari hii mara mbili zaidi
ilidhihirishwa pia baada ya kutoa hesabu ya safu kubwa ya vigezo vingine
vinavyohusiana na hatari kubwa ya kuaga dunia.
Watafiti hao hawakupata ushirikiano
kati ya muda unaotumiwa na mtu anapotumia tarakilishi au kuendesha gari
na hatari kubwa ya kuaga dunia mapema kutokana na sababu zote.
Pia waliongezea kuwa utafiti zaidi
unapaswa kufanywa ili kudhibitisha ni athari zipi zilizopo kati ya
kutumia tarakilishi na kuendesha gari katika viwango vya vifo, na pia
kutathmini taratibu za kibayolojia zinazoweza kueleza uhusiano huo.
"Watu wanapoendelea kuzeeka, tabia za
kukaa tu zitaenea zaidi, hasa kutazama runinga, na hili litasababisha
mzigo mkubwa katika ongezeko la matatizo ya kiafya yanayoambatana na
kuzeeka," Martinez-Gonzalez alisema.
"Matokeo ya utafiti wetu yanapendekeza
watu wazima wajihusishe katika mazoezi ya viungo, waache kukaa tu kwa
muda mrefu, na wapunguze kutazama televisheni kwa zaidi ya saa mbili
kila siku."
BBC
Post a Comment