Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

AJERUHIWA NA WEMBE AKISHUTUMIWA UGONI

 

Mkazi mmoja wa Mtaa wa Msamvu B mjini hapa,  Rehema Juma amekatwakatwa na wembe shavuni na mkononi kisha kuvuliwa nguo na kupigwa na jirani yake akimtuhumiwa kutembea na mumewe.Tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita mnamo saa 11:00. Mwanamke huyo alidai kuwa kabla ya kujeruhiwa aliitwa na jirani huyo na bila kujua alichoitiwa, alikwenda nyumbani kwa mwanamke huyo ambako alifungiwa ndani.Alisema akiwa ndani jirani huyo alimtuhumu kufanya mapenzi na mume wake na hata alipojaribu kukataa, alitishia kumuua.“Kwa kuhofia kuuawa niliona nikubali tuhuma hizo na aliniuliza ni mara ngapi nilifanya mapenzi na mume wake na kama nilikuwa napewa pesa, hivyo nilikiri kufanya mapenzi mara mbili na kwa mara ya kwanza alinipa Sh2,000 na mara ya pili alinipa Sh5, 000 na baada ya hapo aliniachia na nikarudi nyumbani,” alidai Rehema.
Rehema aliendelea kudai kuwa siku hiyo mnamo saa 11:00 jioni binti wa mwanamke huyo alifika tena nyumbani kwake na kumwambia anaitwa tena na mama yake. Naye bila ya hofu alikwenda nyumbani kwa mwanamke huyo na alipofika aliingizwa kwenye chumba kimoja ambacho alikuwamo mume wa mwanamke huyo na kuanza kumpiga, akamvua nguo na kumkatakata kwa kiwembe shavuni na mikononi.
Alidai kuwa baadaye mwanamke huyo alianza kumpiga mume wake, lakini mwanaume huyo alichomoka na kukimbia na alipomkimbiza ndipo yeye alipopata nafasi ya kutoka nje akiwa amebaki hana nguo huku akichuruzika damu.
 Aliporudi nyumbani kwake, Rehema alisema aliongozana na mume wake Godfray Shichonge na ndugu zake wengine kwenda polisi kutoa taarifa na baadaye walipewa PF3 kwenda kutibiwa.
Godfray Shichonge, ambaye ni mume wa Rehema alidai kuwa tangu alipoanza kuishi na mkewe hajawahi kusikia taarifa zozote za kufanya mapenzi nje ya ndoa yao na kuwa katika mtaa huo ni wageni na hawana mazoea na mtu yeyote.
“Alipoitwa nyumbani kwa mama huyu na kufanyiwa ukatili aliniacha nyumbani nikiwa nimepumzika na kabla ya kuondoka aliniaga na nikadhani kuwa ni masuala ya kawaida ya kina mama. Ghafla nilishtuka usingizini kutokana na kilio cha mke wangu aliyerudishwa nyumbani akiwa anavuja damu na akiwa amevuliwa nguo zote,” alisema Shichonge.
Alisema kitendo alichofanyiwa mke wake ni udhalilishaji kwani hata kama mwanamke huyo alikuwa akimtuhumu kufanya mapenzi na mume wake alipaswa kufuata sheria na siyo kumjeruhi kwa kumkata kwa viwembe na kumvua nguo.
Mjumbe wa mtaa huo, Dimoso Frances alisema baada ya mwanamke huyo kumkatakata mwenzake kwa viwembe, alikwenda nyumbani kwa mjumbe huyo na kuomba asamehewe kwani alifanya hivyo kutokana na hasira.
Dimoso alidai kuwa kutokana na hali ya majeruhi kuwa mbaya, hakuweza kutoa uamuzi wowote na hivyo aliamua kufuatilia taarifa hizo polisi ambako aliambiwa kuwa tayari kesi ya kujeruhi ilishafunguliwa kwa jalada namba MORO/IR/4009/2014.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top