STAA
wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel ameshindwa kutimiza azma yake ya
kufuturisha pamoja na kuwaombea dua wasanii walioaga dunia kutokana na
kuugua na kulazwa.
Staa wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel.
Awali msanii huyo alitangaza kufanya tukio hilo Jumanne iliyopita
lakini Mungu hakutaka atimize lengo lake hilo kufuatia kukumbwa na
malaria ya nguvu pamoja na presha.
“Nasikitika sana nimeshindwa kutimiza lengo langu maana niliugua ghafla na kulazwa Hospitali ya Dk. Mvungi, sikuwa na cha kufanya zaidi ya kumuomba Mungu anijaalie uzima ili niweze kutimiza lengo hilo siku nyingine kabla Ramadhani haijaisha,” alisema Aunt.GPL

Post a Comment