Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

CHADEMA Yamwangukia Msajili wa vyama vya Siasa.....Yamtaka asaidie kuruhusiwa kufanyika kwa mikutano ya hadhara



Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Mtwara, Kassim Bingwe, amemuomba msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, kuzungumza na serikali ili ione umuhimu wa kusitisha amri yake ya marufuku ya mikutano ya hadhara katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Mwito huo ameutoa juzi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mtwara (MTPC).
Alisema kwa kufanya hivyo atakuwa anatetea demokrasia ambayo inatoa haki kwa wote kusikilizwa na kufanya mikutano ya hadhara.
“Tunaomba Msajili wa Vyama vya Siasa aachane na mambo ya ndani ya chama chetu kwa sasa yeye analo jukumu kubwa la kuongea na mamlaka za juu za serikali ili amri ya kupiga marufuku kwa mikutano ya hadhara iondolewe hivyo nasi tupate haki ya kufanya mikutano na kuongea na wanachama wetu", alisema Bingwe.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa wao kama chama mara kadhaa wameiomba serikali kuondoa amri hiyo kwani sasa hali ya amani imerejea katika mikoa hiyo lakini bado haijatekeleza ombi hilo hivyo ni nafasi ya msajili kuitumia nafasi hiyo kwani anawajibika pia kuona vyama vikifanya mikutano katika maeneo yote ya nchi kama ilivyo sheria anayoisimamia.
Mikoa ya Lindi na Mtwara iliwekewa marufuku ya kutofanya mikutano ya hadhara ya kisiasa na mingineyo kwa muda usiojulikana kutokana na vurugu zilizojitokeza mwanzoni mwa mwaka jana zilizosababishwa na kundi la baadhi ya wakazi wa mikoa hiyo kupinga mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara kuja Dar es Salaam.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top