Rais
Jakaya Kikwete (katikati) akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mradi
mkubwa wa Maji kwa upande wa Wilaya ya Nachingwea katika Kijiji cha
Chiumbati mkoani Lindi. Mradi huo mkubwa wenye thamani ya Shilingi
Bilioni 34.6 pia unajumlisha Wilaya ya Masasi iliyopo Mkoa wa Mtwara.
Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo
la Nachingwea, Mathias Chikawe. Wapili kushoto ni Waziri wa Maji, Prof
Jumanne Magembe, na kushoto ni Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete. Picha na
Felix Mwagara wa WMNN.
Rais
Jakaya Kikwete akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Chiumbati wilayani
Nachingwea baada ya kuzindua Mradi Mkubwa wa Maji kwa upande wa Wilaya
ya Nachingwea, Mkoa wa Lindi. Mradi huo mkubwa wenye thamani ya Shilingi
Bilioni 34.6 pia unajumlisha Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara. Kushoto
aliyekaa ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa
Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akifuatiwa na Waziri wa Maji, Prof
Jumanne Magembe. Picha na Felix Mwagara wa WMNN.
Rais
Jakaya Kikwete akimtwisha ndoo ya maji Mkazi wa Nachingwea mjini mara
baada ya kuzindua mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya Shilingi Bilioni
34.6 unaojumlisha Wilaya ya Nachingwea na Masasi mkoani Mtwara. Kulia
ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Nachingwea, Mathias Chikawe akifuatiwa na Waziri wa Maji, Prof Jumanne
Magembe. Picha na Felix Mwagara WMNN.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,
Mathias Chikawe akimshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kuzindua Mradi
Mkubwa wa Maji jimboni kwake Nachingwea mkoani Lindi. Mradi huo wa Maji
wenye thamani ya Shilingi Bilioni 34.6 unajumlisha Wilaya ya Nachingwea
na Masasi iliyopo Mkoa wa Mtwara. Katika hotuba yake fupi ya kumshukuru
Rais Kikwete, Waziri Chikawe alisema jimbo lake lilikuwa linateseka na
shida ya maji kwa kipindi kirefu lakini sasa tatizo hilo limekwisha.
Picha zote na Felix Mwagara wa WMNN.
Post a Comment