Wanafunzi
wa Chuo cha Uuguzi cha Huruma ya Mungu Yatosha kilichogundulika kuwa
ni feki katika kata ya Nyehunge wilayani Sengerema wakiwa ndani ya
darasa lao huku wakiwa wamejawa na majonzi baada ya kutapeliwa.(picha na
Daniel Makaka Sengerema).
Na Daniel Makaka, Sengerema
MKUU
wa wilaya ya Sengerema, Bi Kalen Yunus amekifunga chuo cha uuguzi cha
Huruma ya Mungu Yatosha baada ya kukiukwa kwa taratibu za usajili.
Mkuu huyo aliamua kukifunga chuo baada ya kupata taarifa za chuo hicho kuendeshwa bila usajili.
Pamoja
na kufungwa kwa chuo hicho, wanafunzi wake wanaiomba serikali iwasaidie
kurejeshewa fedha walizotoa katika chuo hicho kutokana na mwenye chuo
kuwadanganya kuwa kimesajiliwa wakati akijua si kweli.
Wamesema
walijiunga hapo baada ya kuona matangazo mbali mbali kuhusu chuo hicho
kuwa kinatoa mafunzo ya uuguzi na maabara na kwamba inachukua watu wa
kidato cha nne bila kujali matokeo.
Jengo
la chuo feki cha Uuguzi (nursing) cha Huruma ya Mungu Yatosha
kilichopo kata ya nyehunge wilayani Sengerema.
Baada
ya kupata matangazo hayo yaliyokuwa na namba za simu waliamua kupiga
simu ili kupata maelekezo juu ya kujiunga na chuo hicho maelekezo
waliyopewa ni kufika chuoni wakiwa na karo pamoja na fedha kwa ajili ya
sale za shule.
Wamefafanua
kuwa baada ya kufika chuoni hapo , kata ya Nyehunge wilayani humo
mazingira ya chuo hicho yalikuwa na utata kutokana na kutokuwa na
madarasa ya kutosha na wakazi wa maeneo hayo kutokuwa na taarifa ya
uwapo wa chuo hicho na kuwashangaa wanafunzi hao.
Wamefafanua
kuwa baada ya kukaa kwa muda mfupi mabadiliko mbali mbali yalikuwa
yanafanyika katika chuo hicho huku wanafunzi wakifukuzwa pasipo
utaratibu kitendo ambacho kiliwatia shaka.
Aidha chuo hicho kilikuwa na mwalimu mmoja tu aliyekuwa anafundisha tangu kuanzishwa kwake mwaka 2013.
Wanafunzi wakiwa na majonzi ya baada ya kutapeliwa.
Pia
wamesema kuwa baada ya kujua kuwa chuo hicho bado hakijasajiliwa
walimwomba mmiliki wake kuzungumza nao ili kupata mwafaka wa swala hilo
lakini alikata katakata na kuwatishia kuwafukuza endapo wakiendelea
kumfuatafuata.
Kwa
upande wake mmiliki wa chuo hicho Bw, Ballu Clavery amekiri wazi kuwa
chuo hicho hakijasajiliwa na alitumia namba ya zahanati iliyokuwa
inamilikiwa na mjomba wake ili kuanzisha chuo hicho.
Hata
hivyo alivyoulizwa na waandishi wa habari juu ya hatima ya wanafunzi
hao amesema kuwa atakaana nao ili waweze kupata ufumbuzi wa suala hilo.
Post a Comment