Imetolewa leo tarehe 16 Julai
2014
Na Dismas Lyassa
Mgombea Urais wa TUCTA; Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi
Mgombea Urais wa TUCTA; Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi
Salaam
Shukrani
Ndugu wanahabari
Nawapenda
kuwashukuru kwa ujio wenu. Nichukue fursa hii niwatambulishe walioko mbele yenu
ili kufahamiana. Nianze kwa kujitambulisha mimi mwenyewe, naitwa Dismas Lyassa,
ni mwandishi wa habari mwenzenu…nimekuwa katika hii kazi kwa miaka 20 sasa na
nimewahi kufanyia kazi katika magazeti mbalimbali yakiwamo Alasiri, Financial
Times, Leo ni Leo na tangu 2005 nimekuwa nikifanyia kazi katika gazeti la
Mwananchi hadi sasa nikiwa mhariri anayeshughulikia masuala ya biashara na
uchumi. Pia toka mwaka 2012 nilichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa COTWU tawi la
Mwananchi Communications Limited, nafasi ambayo kisheria mtu anapaswa kudumu
kwa miaka mitano, lakini akitaka anaweza kugombea.
Utambulisho
Ndugu wanahabari
Wengine
niliombatana nao ni mke wangu Mchungaji Rightess Lyassa wa Kanisa la Ufufuo na
Uzima, Kawe -Dar es Salaam, Mussa Mwakalinga Katibu Mkuu wa Chama cha
Wafanyakazi wa Mawasiliano na Usafirishaji (COTWU) kanda ya Dar es Salaam,
wakili wangu Jebra Kambole kutoka kampuni ya Uwakili ya Law Guards ya Jijini
Dar es Salaam, na meneja kampeni Khamis Tembo.
Ndugu wanahabari
Lengo
hasa la kuwaiteni mahali hapa ni kutoa taarifa kwenu kuwa ninagombea Urais wa
Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania, uchaguzi ambao unatarajiwa
kufanyika Agosti 4-5, Dodoma.
Vipaumbele vyangu
ni vyangu
Ndugu wanahabari
Nina
malengo ya kuifufua na kuleta TUCTA yenye uhai na mabadiliko ya kweli kwa
kufanya yafuatayo;
Ndugu wanahabari
1. Kupigania na
kulinda haki za wafanyakazi;
Katika
kipaumbele hili lengo hasa ni kuondoa matatizo sugu ya wafanyakazi yakiwamo-:
i.
Kulipwa
ujira/mishahara duni isiyoendana na uhalisia wa maisha.
ii.
Ucheleweshaji
wa upatikanaji wa ujira/mishahara
iii.
Ucheleweshaji
fedha za kujikimu kwa waajiriwa wapya/ kiwango kidogo cha fedha za kujikimu
iv.
Uhaba
au kutokuwepo kabisa makazi kwa wafanyakazi wapya
v.
Rushwa
na kuajiri kwa misingi ya kujuana kwa mfano katika Halmashauri ya Siha, wilaya
ambayo imegawanywa kutoka Hai, kuna pori kubwa la West Kilimanjaro mlimani
kabisa, hakuna maendeleo…ni suala la kawaida kuona watu wakiongea kilugha
ofisini kama lugha ya Taifa
vi.
Wakubwa
yaani mabosi kujifanya Mungu kwa kuwaendesha wafanyakazi kwa kadri wanavyotaka
wao, sivyo inavyosema sheria.
vii.
Uwepo
wa mpangilio usio sawa wa ujira/mishahara.
viii. Kutopewa posho au kupewa kidogo
au kutopewa kwa wakati
ix.
Fedha
za uhamisho na likizo; kwa mfano kuna walimu ambao wameanza kazi 2004 NIT Shule
ya msingi Dar es Salaam wamelipwa fedha za likizo mara moja mwaka 2012, mfano
halisi ni mwalimu Ruth Natumwa, huyo ni kati ya walimu hao. Matatizo ya walimu
kimsingi ni janga la taifa, yapo Taifa zima, kwa mfano katika shule ya
Sekondari Kizota, Dodoma kuna walimu wengi
wana madai yao dhidi ya Serikali, waliajiriwa mwaka jana Machi, wakaanza
kupata mshahara mwenzi wa tisa…walilipwa mshahara wa mwezi wa tisa tu na
kuendelea, ile mingine wanaendelea
kudai.
x.
Mazingira
magumu ya kazi mijini na vijijini (tunapozungumzia mazingira magumu inahusisha
kutokuwepo vitendea kazi au kuwa vichache, miundo mbinu duni nk).
xi.
Waajiri
kutochangia mifuko ya jamii
xii.
Fedha
za makato ya wafanyakazi kupitia mifuko ya jamii zimekuwa zikikopeshwa watu
wengine wasio wanachama wakiwamo wanasiasa huku wafanyakazi wenyewe wakiendelea
kuwa na maisha duni
xiii. Kufanya kazi kama kibarua kwa
miaka mingi jambo ambalo ni tofauti za sheria za kazi
xiv. Huduma za kifedha kuwa mbali na
maeneo ya kazi, hali inayosababisha wafanyakazi kutumia fedha nyingi kufuatilia
mishahara kwa vile ni mbali na eneo wanalofanyia kazi.
xv.
Kutokuwa
na mfumo unaoeleweka wa upandishaji vyeo na ujira/malipo kwa
wafanyakazi/vibarua
xvi. Waajiri hasa binafsi kufukuza
wafanyakazi hovyo/no job security…kufanya kazi bila mikataba
xvii. Kupambana na tatizo la kodi
kubwa kwa mishahara (PAYE)
xviii. Tatizo la mabosi kutoa
upendeleo wa wazi kwa baadhi ya wafanyazi kwa sababu zisizo za kitaalamu;
wakati mwingine ni kwa sababu ya ngono; kuwataka kimapenzi wafanyakazi ili
waendelee kuwepo kazini au kupandishwa vyeo…tatizo hili linaonekana kuwa sugu,
wanawake wengi maofisini hawako huru sana, wamekuwa wakitakwa kimapenzi mno na
mabosi wao, wengi wanashindwa kujizuia, tunataka kuona kunakuwa na sheria kali
dhidi ya mabosi wa aina hii kama ilivyo katika nchi nyingine.
Ndugu wanahabari
Tatizo la ajira
kuporwa na wageni
Ingawa sheria/sera za ajira zinaeleza wazi
kwamba hairuhusiwi wageni kuingia nchini zaidi ya watano kwa kazi ziziso na
ujuzi, baadhi ya makampuni yamekuwa yakiingiza wageni kwa kazi ambazo
Watanzania wengi wanaweza kuzifanya.
Ndugu wanahabari
Nitahakikisha wazawa wanapewa fursa ya kufanya kazi nchini; hii ni pamoja na kuomba CV za wageni ili tuone kama ni kweli hakuna Watanzania wenye sifa za kufanya hiyo kazi hiyo.
-: Kumekuwa na taarifa za uwepo wageni katika makampuni kadhaa yakiwamo mahoteli, migodi, viwanda vya sarufi nk ambao baadhi wanalipwa malipo makubwa tofauti na wazawa japo hawana elimu au ujuzi wa kuwazidi wazawa. Nitakuwa na kamati maalumu ya kufuatilia waajiriwa wote Tanzania hasa wageni ili kujua kama wanazo sifa za kufanya kazi au wanapora nafasi za Watanzania.
Nitahakikisha wazawa wanapewa fursa ya kufanya kazi nchini; hii ni pamoja na kuomba CV za wageni ili tuone kama ni kweli hakuna Watanzania wenye sifa za kufanya hiyo kazi hiyo.
-: Kumekuwa na taarifa za uwepo wageni katika makampuni kadhaa yakiwamo mahoteli, migodi, viwanda vya sarufi nk ambao baadhi wanalipwa malipo makubwa tofauti na wazawa japo hawana elimu au ujuzi wa kuwazidi wazawa. Nitakuwa na kamati maalumu ya kufuatilia waajiriwa wote Tanzania hasa wageni ili kujua kama wanazo sifa za kufanya kazi au wanapora nafasi za Watanzania.
Ndugu wanahabari
Nitapigania
kuhakikisha tabia ya waajiri kulazimisha waajiriwa lazima wawe na uzoefu mkubwa
inapungua au kukoma kabisa
Kigezo cha kupata ajira kiwe ni uwezo wa mtu
wakati huo baada ya kufanyiwa usaili, siyo lazima awe na uzoefu wa miaka mitatu au mitano kama ambavyo
waajiri wengi wanalazimisha; tunahitaji kuona Serikali inasimamia hili. Kama
hali ni hii, wahitimu wanawezaje kupata ajira? Ni suala ambalo nitakuwa mkali
nalo mno kwa sababu lina athari kubwa kwa jamii ya Tanzania, limekuwa ni sababu
ya rushwa ikiwamo ya ngono…walioko vyuoni wengi hawana uhakika wa ajira, kwa
sababu ya tabia hii. Ni lazima tubadilike, watu waajiriwe kulingana na uwezo
wao wa kazi, siyo uzoefu.
Ndugu wanahabari
Wanafunzi shule
ya Msingi/Sekondari nk wapatiwe elimu ya kujiajiri.
Kwa nafasi nitakayokuwanayo nitaishawishi Serikali iingize elimu ya ufundi/utengenezaji bidhaa na ujasiriamali kama mojawapo ya masomo ya ziada kama njia ya kupambana na tatizo la ajira ambalo linaonekana kukua nchini. Kama ambavyo kumekuwa na masomo ya dini katika shule zenu, tuwe pia na masomo ya ujasiriamali. Nitaangalia namna ya kuzishawishi taasisi zingine za ndani na nje kuhakikisha hili linafanyika; lengo ni kuhakikisha hata mhitimu wa msingi au sekondari nk awe ana uwezo wa kufanya ujuzi anaotaka kama kujenga, kushona, kufuma, kufuga, kutengeneza batiki, vikoi, sabuni, mishumaa nk.
Kwa nafasi nitakayokuwanayo nitaishawishi Serikali iingize elimu ya ufundi/utengenezaji bidhaa na ujasiriamali kama mojawapo ya masomo ya ziada kama njia ya kupambana na tatizo la ajira ambalo linaonekana kukua nchini. Kama ambavyo kumekuwa na masomo ya dini katika shule zenu, tuwe pia na masomo ya ujasiriamali. Nitaangalia namna ya kuzishawishi taasisi zingine za ndani na nje kuhakikisha hili linafanyika; lengo ni kuhakikisha hata mhitimu wa msingi au sekondari nk awe ana uwezo wa kufanya ujuzi anaotaka kama kujenga, kushona, kufuma, kufuga, kutengeneza batiki, vikoi, sabuni, mishumaa nk.
Ndugu wanahabari
Nitaanzisha idara
mbili mpya na kuboresha zilizoko;
i. Idara ya walemavu
Hii itahusika kuangalia hali ya maisha ya wafanyakazi walemavu nchini ikiwamo kuwasaidia kupata baiskeli na huduma zingine muhimu.Nitatumia uzoefu wangu kwa kushirikiana na rafiki zangu wa nje kuhakikisha hili linafanikiwa. Tutaangalia namna ya kushirikiana na mashirika mbalimbali yakiwamo Free Wheelchair Foundation www.wheelchairfoundation.org.
i. Idara ya walemavu
Hii itahusika kuangalia hali ya maisha ya wafanyakazi walemavu nchini ikiwamo kuwasaidia kupata baiskeli na huduma zingine muhimu.Nitatumia uzoefu wangu kwa kushirikiana na rafiki zangu wa nje kuhakikisha hili linafanikiwa. Tutaangalia namna ya kushirikiana na mashirika mbalimbali yakiwamo Free Wheelchair Foundation www.wheelchairfoundation.org.
Ndugu wanahabari
Kutakuwa
ni mikakati mbalimbali kuhusu wafanyakazi walemavu na wale wanaopata ulemavu
wakiwa kazini, kwa mfano Mwenyekiti wa Wasioona mkoani Tanga amekuwa ni mtu
ambaye ameumia kazini, lakini aliishia kulipwa Sh150,000 na bandari ambako
alikuwa anafanya kazi kama kibarua.
Kitendo kitakuwa na jukumu la kufuatilia kwa ukaribu hali za wafanyakazi
walemavu, kuangalia kama wanavyotoka vyuoni wanapewa ajira au wanaishia
kunyanyapaliwa? Utafiti unaonyesha kuna wanafunzi wengi wanaohitimu masomo
wakiwa na ulemavu, hata hivyo hawaonekani kwenye maofisi wakifanya kazi.
Wanakwenda wapi? Litakuwa ni jukumu la hicho kitengo.
Ndugu wanahabari,
Idara ya pili ni
Idara ya
fursa/Career Development Department na Mafunzo
Nimetembea katika nchi tofauti Duniani ikiwemo
Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Mauritius, India, Thailand, Sweden na
Marekani…nimeona fursa kadhaa ambazo zimenishawishi kuanzisha idara maalum ya
kusaidia wafanyakazi kufahamu fursa zinazoendelea Duniani na hapa nchini. Fursa
hizo zitakuwa zinapatikana katika tovuti za TUCTA na ofisi za vyama vya
wafanyakazi mikoani. Baadhi ya fursa ni namna gani mtu anaweza kusoma nje ya
nchi bila kulipa ada kwa kozi za muda mrefu na mfupi, fursa ya mashirika ambayo
yanatoa misaada kwenye sekta mbalimbali.
-Kwa
mfano kuna mashirika kama www.nuffic.nl au vyuo ambavyo mtu anaweza
kusoma bure bila kulipa chembe ya ada kama www.berea.edu ya Marekani na fursa nyingine nyingi.
Nimegundua Watanzania wengi hawanufaiki sana na fursa hizi. Ziko pia taasisi
nyingine zinatoa.
Ndugu wanahabari
Idara
hii itakuwa na majukumu ya kutoa elimu kwa wafanyakazi kuzifahamu sheria za
kazi, hali kadhalika itakuwa inawasiliana na waajiri ili zaidi ya barua ya
ajira au mkataba wanaompa mwajiriwa, ampe pia na chapisho letu ambalo mwajiriwa anapaswa
kupewa siku ya kuajiriwa kwake ili ajue kwa uhakika sheria za kazi zinasemaje;
haki ya mwajiriwa kwa mwajiri au ipi na haki ya mwajiri kwa mwajiriwa ni ipi;
tutashawishi hili liwe ni suala la lazima. Tutakuwa na vituo maalum vya msaada
wa kisheria mikoani kote au kwenye kanda. Tutakuwa na vipindi kwenye
televisheni angalau kila mwezi mara kuelezea masuala ya sheria za kazi.
Tutaitumia tovuti ya TUCTA kuwa ya
kisasa zaidi.
Ndugu wanahabari
Kulifufua gazeti la Mfanyakazi ndani ya siku
90 ili liwe sauti thabiti ya wafanyakazi
Haijalishi
kama TUCTA itakuwa na fedha au la, nitahakikisha ndani ya siku 126 litakuwa mitaani likiandika habari mbalimbali
hasa likitumika kama sauti ya wafanyakazi na yote ambayo yataonekana ni ya
maana kwa ustawi wa taifa. Nina uzoefu zaidi ya miaka 20 katika sekya ya habari
kama Mhariri, na hata sasa ni Mhariri wa Biashara gazeti la Mwananchi,
nitahakikisha tunatafuta fedha ndani na nje ya TUCTA ikiwamo kuwatumia
wafanyabiashara kwa kubadilishana msaada kwa matangazo kwa muda, ili hatimaye
liweze kuwa mitaani. Ni aibu kubwa kuona nchi ina wafanyakazi wengi, lakini
gazeti kama hili la wafanyakazi haliko mitaani.
Ndugu wanahabari
Kuimarisha uhusiano wa vyama vya ndani na
vyama vya nje
Nitahakikisha
nafanya mawasiliano na mashirika mengine yakiwamo International Trade Union
Confederation, Secretary General Sharan
Barrow na mashirika mengine ili kuona namna gani vyama vya wafanyakazi
vya nchini vinanufaika na ushirikiano huo kwa kubadilishana uzoefu na kadhalika
mara kwa mara kadri inavyowezekana.
Ndugu wanahabari
Nitatutumia
uzoefu wangu wa shughuli za kuwasiliana na vyuo vya nje na uzoefu wangu wa
kufanya kazi katika mashirika mbalimbali ya nje kama muwakilishi wao hapa
nchini, na kutembea nchi mbalimbali,
kuviunganisha vyama vya ndani vya wafanyakazi, kuwa na ukaribu zaidi na vile
vya nje, na pia kujenga uwezekano wa viongozi nchini kwenda nje kupitia
ushirikiano huo.
Ndugu wanahabari
Hili
linawezekana kwa njia mbili, kwanza kama washirika wetu kwa vile tutakuwa tuna
mawasiliano ya karibu na aina ya chama ambacho mtu anatoka, kwa mfano kama
COTWU, TTU, TALGWU, TUICO, TAMICO, TEWUTA, DOWUTA, TPAWU, RAAWU, TUGHE,
CHODAWU, TRAWU. Nahitaji kuona ofisi za vyama vya wafanyakazi nchini zinakuwa
za kuvutia kwa kuzipatia vitendea kazi, kuna mashirika nayafahamu, tunaweza
kuyatumia kuwasiliana nayo yakatusaidia kama vile Computer Aid International la
Uingereza ambalo hutoa misaada ya computer za aina mbalimbali kwa nchi maskini
kama Tanzania (www.computeraid.org). Nje ya hiyo nitakuwa na
vikao na viongozi wa chama kimoja badala ya kingine kuangalia namna gani
tunaweza kuboresha shughuli za utendaji za ndani na nje hasa kuimarisha
rasilimali watu na vifaa. Lengo kubwa la kuomba niwe Rais wa TUCTA ni kuangalia
namna gani tunaweza kushirikiana na wafanyakazi na viongozi wa vyama katika
kuimarisha wafanyakazi, kwani malalamiko ni mengi. Tutaendeleza
mali za TUCTA zikiwamo Chuo cha Wafanyakazi Mbeya na maeneo mengine.
Ndugu wanahabari
NAMNA GANI HAYA
YATAWEZEKANA?
Mkakati
wa kuondoa kero zote zilizoelezwa juu utafanikiwa kwa majadiliano yenye ukomo
(deadline) na Serikali/waajiri, au kufanya chochote ambacho katiba inaruhusu.
Sheria ziko wazi, nitahamasisha zifuatwe na zifahamike. Shida kubwa ninayoiona
kwa sasa, wafanyakazi wengi hawajui haki zao pia msaada wa vyama katika
kuwasaidia wafanyakazi ni mdogo.
Ndugu wanahabari
Hata
hivyo mkakati hasa ni kuangalia TUCTA kwa kushirikiana na vyama shiriki
vinafanya nini kuondoa changamoto ambazo sisi wenyewe tunaweza kuziondoa.
Uongozi siyo kulalamika, bali kuthubutu kuchukua hatua zinazoweza kuondoa shida
zilizoko. Tayari nimeanza kuwasiliana na vyama mbalimbali vya wafanyakazi katika
mataifa ya nje ili kuangalia namna gani tunashirikiana kwa maana ya
kubadilishana uzoefu nk.
Ndugu wanahabari
Ofisi
nyingi za vyama vya wafanyakazi zimechakaa, naangalia uwezekano wa kushirikiana
nao katika hili kwa njia ya kutafuta wafadhili wa nje au kubuni miradi
itakayosaidia kuondoa hali hiyo; nataka pia maisha ya viongozi wa vyama vya
wafanyakazi na wafanyakazi kwa ujumla yabadilike kwa kutumia jitihada hizo
nilizozieleza juu, nafahamu vizuri namna ya kusaka wafadhili, kwani ni shughuli
ambayo nimekuwa nikifanya kwa muda mrefu kupitia taasisi yangu ya Global Source
Watch, niliyoianzisha toka mwaka 2001 ambayo imekuwa ikifanya kazi ya
kuwaunganisha watu na vyuo zaidi ya 78 vya nje kama Marekani, Canada, Greece,
India, Malaysia nk.
Ndugu wanahabari
Nafahamu
kuna vyama vina miradi ya maendeleo, vinawasaidiaje wanachama wao? Nahitaji
niwe Rais ili nishirikiane na vyama vya wafanyakazi na wafanyakazi kwa ujumla
kuleta tija kwa Watanzania. Tusiwe watu wa kunyoosheana vidole…kila mtu awe
chanzo cha mabadiliko anayotaka kuyaona Tanzania! Naamini kila mtu akifanya
kazi zake vizuri…Tanzania itakuwa na maendeleo kwa kasi. Wafanyakazi wanahitaji
mambo mengi zaidi ya kuhamasishwa migomo, lakini kama tutaamua kugoma,
tunapaswa kugoma kwa kumaanisha, hatupaswi kuogopa kutekeleza yaliyo haki yetu.
Ndugu wanahabari
Kwa
nafasi nitakayokuwa nayo nitaanzisha semina, makongamano, mijadara itakayokuwa
ya wazi na kutoa elimu ya kutosha juu ya haki za wafanyakazi na wajibu wa
waajiri kwa wafanyakazi. Hii itasaidia kupunguza migogoro na wafanyakazi
watatambua haki zao.
Ndugu wanahabari
Tunatakiwa
kuwa sauti ya wafanyakazi hapa Tanzania, TUCTA imelala, tunataka kuikimbiza
mchakamchaka,, kuna mambo mengi yanatokea dhidi ya wafanyakazi hapa nchini
lakini TUCTA haitoi hata matamko au kutetea wafanyakazi,
Ndugu wanahabari
Natambua
changamoto za wafanyakazi, tunataka kuwa na
TUCTA
Mpya
Nguvu
Mpya
Uongozi
Mpya
Sauti
Mpya
Umoja
Mpya
Maendeleo
Mapya
Kwa
pamoja tunaweza.
Mungu
awabariki!
Dismas
Lyassa
Mgombea
nafasi ya Urais-TUCTA
simu 0754 49 89 72
simu 0754 49 89 72
--------------------------------------------------------------------------------------------------
HOTUBA FUPI KUTOKA KWA JEBRA
KAMBOLE, Wakili wa Dismas Lyassa anayefanya Kampuni ya Uwakili ya Law Guards
Advocates ya Jijini Dar-es-salaam kwa Waandishi wa Habari.
Ndugu
waandishi wa Habari wa vyombo vyote vya Habari,
Ndugu
watanzania wengine mliopo hapa,
Shukrani
Tunashukuru
sana kwa kuitikia wito wetu, Mungu awabariki sana, Tunamshukuru mwenyezi mungu
kwa kutupa afya na sia njema,
Ndugu waandishi wa Habari
Kuna
mambo muhimu manne tunataka kuwaeleza watanzania wote, hasa wafanyakazi na
viongozi wa vyama vyote vya wafanyakazi
Moja,
Ndugu anatimu iliyojipanga makini kuhakikisha TUCTA inarejea na kuwa na Nguvu
zaidi, Ni kijana makini mwenye malengo ya kuleta maendeleo ya haraka na kufufua
uhai wa TUCTA.
Ndugu Waandishi wa Habari
Napenda
kuchukua fursa hii kutoa onyo kwa wanaopanga kutoa rushwa kwenye huu uchaguzi
wa TUCTA kuwa tuko makini na hili tumejipanga, tutachukua hatua za haraka za
kisheria dhidi yao, ikiwa ni pamoja na kuwaripoti kwenye vyombo husika, Rushwa
si kipaumbele utapinga kwa nguvu zetu zote.
Ndugu Waandishi wa Habari
Ndugu
Dismas Lyasa pia atasaidia kuanzisha kituo au kushirikiana na mashirika mengine
kutoa masaada wa kisheria kwa wafanyakazi wanaofukuzwa makazini kinyume cha
sheria. Wafanyakazi wengi wakikumbwa na matatizo wafanyakazi wenzao
wanawatenga, vyama vyao vinawatenga, Dismas atahakikisha kuwa TUCTA ni kimbilio
lao.
Ndugu Waandishi wa Habari
Ndugu
Dismas Lyasa atasaidia kutoa mafunzo ya kisheria kwa wafanyakazi ili waweze
kutambua haki zao za msingi, kwa kuendesha semina, makongamano na mijadara
itakayotoa elimu na kuibua mijadara kwa wafanyakazi.
CHAGUA
DISMAS LYASA KWA TUCTA MPYA, Mabadiliko ni sasa,,,Asanteni
Post a Comment