MBUNGE wa Kigoma Kusini kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, David Kafulila, amesema haogopi kushtakiwa na kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited ( IPTL) kwani hata watu wasio na haki wana ujasiri wa kwenda mahakamani.
Hayo yamebainishwa kwenye taarifa iliyotolewa na mbunge huyo kwa vyombo vya habari akidai huo ndio msimamo wake baada ya kupata taarifa kupitia vyombo vya habari kwamba amefunguliwa mashtaka mahakamani kuhusiana na sakata la IPTL.
Jana baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti kuwa Kampuni ya IPTL immemfungulia kesi mbunge huyo katika Mahakama Kanda Kuu ya Dar es Salaam ikimtaka aombe radhi na kuilipa fidia ya bilioni 310. Alisema hawezi kuufumbia macho ufisadi unaofanywa na baadhi ya watu kwa manufaa yao .
“Kwanza Watanzania waelewe kuwa hata wasio na haki wanao ujasiri wa kushtaki ndio maana hata Yesu alishtakiwa, kwa hiyo mimi siogopi vitisho vyao,” alisema Kafulila.
Alisema kwa sasa yuko ziarani mkoani Kigoma kuwaeleza wananchi juu ya mchezo mchafu uliohusisha vigogo wa Serikali na kampuni hizo za PAP na IPTL
“Nasisitiza na nitaendelea kusisitiza kuwa IPTL ni mfululizo wa...hadi mwaka 2013 kwenye utoaji wa fedha za escrow ambazo ni za umma,” alisema Kafulila.
Alisema hukumu ya mwaka 2001 ya mahakama ya usuluishi wa migogoro ya kiuwekezaji ya kimataifa (ICSID) ilitoa hukumu kwamba, IPTL ilidanganya kuhusu aina ya mitambo na ikawa ni ushindi kwa Tanzania, lakini inashangaza kuona bado wanaendelea kukana.
“Naendelea kusema kuwa mchezo huu wa IPTL/PAP ni mchezo mchafu na lazima watu watafungwa hata kama si awamu hii na ipo siku tutapata rais asiye vumilia uchafu na atafukua makaburi yao hata kama wamekufa,” alisema Kafulila.
Post a Comment