Msanii
anaefanya vizuri katika muziki wa R&B Tanzania, Ben Pol ambaye hivi
karibuni alianza kuuza kazi yake ya muziki kwa njia ya mtandao amesema
biashara hiyo ina matunda yanayotia moyo.
Ben
Pol ameeleza hayo alipokuwa anaongea na ENews ya East Africa TV na
alifafanua kuwa ingawa Bongo watu hawajawa na muamko sana wa kununua
kazi za wasanii online lakini msanii akipromote vizuri kazi yake anaweza
kupata hata milioni 6 hadi 7.
“Bado
ni hela ndogo kwa albam ya mauzo ya nyimbo 20, bado sio kivile nafikiri
pia ni kwa sababu watu wanadownload wanashare for free kwa watu
wengini. Lakini kwa sasa hivi kibongobongo unaweza ukauza ukapata
milioni 6 au 7.”
Post a Comment