Je unajua kwamba samaki hasahau?
Mtu
huambiwa ana akili ya kusahau kama samaki. Lakini sasa huenda hilo
likabadilika baada ya wanasayansi kugundua kwamba, kinyume na imani
hiyo, baadhi ya samaki wanaweza kuhifadhi taarifa kuhusu mazingira
waliomo kwa takriban wiki mbili.
Watafiti
kutoka chuo kikuu cha MacEwan, waliwazoezesha baadhi ya samaki wa
Kiafrika wajulikanao kama cichlids, kuingia katika eneo maalum la
tangisamaki ili kupata chakula.
Walitolewa
na siku kumi na mbili baadaye walirudishwa tena ndani ya tangi samaki
hilo, na saamki hao walionekana kuipendelea sehemu hiyo maalum waliokuwa
wakipewa chakula.
Watafiti
hao wanasema ongezeko hilo la muda wa samaki kukumbuka, huenda likampa
samaki nafasi ya kuishi zaidi hususan wakati kuna upungufu wa chakula.
"Samaki
wanaoweza kukumbuka mahali chakula kilipo, wana uwezo wa kuishi zaidi
kuliko wale ambao hawakumbuki," alisema mwandishi mwenza wa ripoti ya
utafiti huo Trevor Hamilton, ambaye ni mwanasayansi wa chuo hicho kikuu
cha MacEwan nchini Canada,
Alisema
samaki wanaweza kukumbuka kwamba sehemu maalum ina chakula bila kuwepo
tishio la samaki wanaoweza kuwaua, na hivyo wataweza kurudi tena katika
sehemu ile.
Wanasayansi
hao wanasema samaki wakiwa baharini, ni muhimu waweze kutambua maeneo
yalio na chakula ili waweze kuendelea kuishi.Chanzo BBC Swahili
Post a Comment