Watu wawili wamekamatwa na Polisi wakihusishwa na
shambulio la bomu lililotokea kwenye mgahawa wa 'Vama Traditional Indian
cuisine' jijini Arusha.
Shambulizi hilo liliyokea Jana siku ya jumatatu saa nne usiku.
Watu wasiojulikana walirusha bomu
ndani ya mgahawa kupitia mlangoni ambapo watu wanane wamejeruhiwa moja
kati yao akiwa na majeraha makubwa.
Aidha,katika matukio mengine, jumla ya Watu 20 wanazuiliwa na Polisi
wakiwemo watu sita wanaosadikiwa kujihusisha na mlipuko wa bomu
uliotokea mkoani Arusha juma lililopita nyumbani kwa Kiongozi wa dini
Sheikh Sudi Ally Sudi na kujeruhi watu wawili.
Polisi wanaendelea na upelelezi kuhakikisha inawatia nguvuni watu waliohusika na matukio hayo.
Haijulikani kilichosababisha mlipuko huo.
Post a Comment