Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KIJANA AKUTWA AMEJIUA KITANDANI HUKO MKOANI GEITA, UGOMVI NA MKEWE WAHUSISHWA NA KIFO HICHO

Mwili wa kijana Paschal Jumbe ukiwa kitandani baada ya kujiua

Kijana aliyejulikana kwa jina la Paschal Jumbe (35) mkazi wa mtaa wa Mission katika kata ya Kalangalala wilaya ya Geita mkoani Geita amekutwa amekufa katika nyumba anayoishi kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni msongo wa mawazo.

Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti wa mtaa huo Juma Kajala amesema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo ambapo saa 2.30 asubuhi alipigiwa simu na watu wanaoishi naye kwenye nyumba hiyo.

Amesema baada ya kufika hapo alikuta dirisha likiwa limefunguliwa na marehemu akiwa amelala kitandani ndipo alipiga simu polisi na walipofika polisi walivunja mlango na kumkuta akiwa amekufa . 

Naye dada wa marehemu Nyanyama Jumbe alisema kuwa mdogo wake alikuwa na ugomvi wa kifamilia na mke wake Reticia Jumbe ambaye walipogombana alikwenda kuishi eneo la Nyankumbu nje kidogo ya mji na huenda ndicho chanzo cha mdogo wake kujinyonga.

Kamanda wa polisi mkoani hapaJoseph Konyo amethibitisha kutokea kwa tukio na kwamba uchunguzi zaidi kuhusu tukio hilo unaendelea
 
Na Valence Robert-Malunde1 blog-Geita
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top