Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KIWANGO CHA MESSI, ROBBEN KUJULIKANA LEO

 


Kiungo mshambuliaji wa timu ya Taifa Uholanzi, Arjen Robben.
Sao Paulo, Brazil
WAKATI  wikiendi ijayo itakuwa siku ya mwisho kwa fainali za Kombe la Dunia, kuna mambo kadhaa yametokea kwenye fainali hizo mwaka huu huku kila shabiki akiwa amejifunza.

Arjen Robben (kushoto) akiwa na Kocha Msadizi wa Uholanzi, Patrick Kluivert.
Fainali hizi zimekuwa na mambo mengi ya kushangaza lakini mwishoni zinaonekana kufika kwenye hatua nzuri na ya heshima, mabingwa watetezi Hispania, timu kubwa kama Ureno, England na Italia ziliondolewa mapema sana.
Kuondoka kwa timu hizi kulifanya fainali hizo zibaki na sura nyingine ngeni kama Chile, Colombia na Costa Rica ambazo zilionyesha uwezo lakini nazo zikaishia njiani.
Leo kwenye Uwanja wa Sao Paulo, kutakuwa na  mechi ngumu na ya heshima, kati ya Argentina na Uholanzi.
Mechi hii inabebwa na wachezaji wawili Lionel Messi wa Argentina na Arjen Robben wa Uholanzi.Chini kuna takwimu za wachezaji hao ambao wote watavaana kwenye mchezo wa nusu fainali leo. Takwimu hizi zinahusu fainali hizo ambazo zimeanza Juni 12 hadi leo.
Lionel Messi wa Argentina.
Arjen Robben:
Mechi alizocheza: 5
Dakika alizocheza: 480
Mabao aliyofunga: 3
Mashuti aliyopiga: 17
Pasi zilizofika: 129
Mipira aliyopokonya: 8
Takolini: 8
Umbali aliokimbia: 55.4 km
Lionel Messi
Mechi alizocheza: 5
Dakika alizocheza: 453
Mabao aliyofunga: 4
Mashuti aliyopiga: 17
Pasi zilizofika: 180
Mipira aliyopokonya: 5
Takolini: 7
Umbali aliokimbia: 41 km


               
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top