Sarafu ya ukumbusho wa goli la kichwa la Van Persie lililoisababishia
ushindi timu yake ya Uholanzi limewekwa kwenye sarafu iliyouzwa ndani
ya saa moja baada ya kuwekwa sokoni.
Van Persie alifunga goli hilo wakati timu yake ilipokutana na
Hispania katika mechi zinazoendelea za Kombe la dunia na kuzua gumzo
kubwa ambapo mashabiki walikuwa wakifanya vitendo mbalimbali kuenzi goli
hilo lililoipa ushindi Uholanzi wa Bao 5-1.
Unaweza kuona kitu cha ajabu lakini ndio hivyo wenzetu wanafanya
hivyo ambapo kampuni iliyopewa mamlaka ya kutengeneza sarafu ilichukua
picha ya kitendo kilichofanywa na nyota huyo wa timu ya Manchester
United Van Persie wakati wa mechi ya ufunguzi wa makundi mwezi uliopita.
Post a Comment