Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Loga amvaa Maximo

 


Kocha Mkuu wa Simba, Mcroatia, Zdravko Logarusic.

Na Martha Mboma
KOCHA Mkuu wa Simba, Mcroatia, Zdravko Logarusic, amesema hamfahamu kocha mpya wa Yanga, Mbrazili, Marcio Maximo, lakini watapambana uwanjani.

Loga, raia wa Croatia, amesema anajua kuwa kocha huyo anatoka Brazil, hivyo hawezi kuwa lelemama, lakini ni vyema wakakutana uwanjani kila mmoja aonyeshe shughuli yake.

Kocha huyo msimu uliopita alikuwa akifahamiana na kocha ambaye amemaliza muda Yanga Hans Van Der Pluijim na waliwahi kufanya kazi pamoja nchini Ghana, lakini Maximo hawana historia hiyo.
Akizungumza  na Championi Jumatano, kutoka nchini Croatia, Loga alisema yeye hawezi kuzungumza lolote kuhusiana na Maximo kwa sababu hamfahamu,  lakini hilo halimuumizi kichwa hata kama nchi yake ina historia nzuri ya soka japo siyo kigezo kikubwa.
 

“Kiukweli huyo kocha mpya wa Yanga, simfahamu na sifahamu chochote kuhusiana na yeye kwa sababu sijawahi kufanya naye kazi lakini tutakutana uwanjani.
“Ingawa anatoka katika nchi yenye historia nzuri ya soka, hilo halijalishi, zaidi tutapambana kila mmoja kuonyesha shughuli yake na ufanisi wa kazi hapo ndiyo utaonekana.
 

“Kikubwa ni kujipanga tu na kuwa na mipango madhubuti ili kuifanikisha timu ingawa hakuna jambo la kuhofia kuwa mtu anatoka nchi fulani, zaidi ni kupambana kufikia malengo, ingawa mpinzani wangu simjui, nitafanya kazi yangu,” alisema Loga ambaye alifanya vizuri kwenye mechi zote alizokutana na Yanga msimu uliopita.

GPL
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top