
Kulia ni Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, akimpongeza Kamanda wa Jumuiya ya Vijana wa CCM(UVCCM) Mkoa wa Mbeya, Yona Sonelo, jana katika viwanja vya mikutano vya Ruanda Nzovwe, Jijini Mbeya.
Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Godfrey Zambi na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa.
Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Dr. Norman Sigalla, akiwa na Katibu wa hamasa na chipukizi Taifa, Paul Makonda, katika viwanja vya CCM Ilomba, Jijini Mbeya jana, wakati wa sherehe za kuapisha makamanda wa UVCCM Mkoa wa Mbeya.
Kushoto ni kamanda wa Jumuiya ya Vijana wa CCM(UVCCM) Mkoa wa Mbeya, Yona Sonelo, akimpa kongole, Kamanda wa UVCCM wilaya ya Mbeya Vijijini, Oran Manase Njeza, baada ya kuapishwa.
Kushoto ni kamanda wa Jumuiya ya Vijana wa CCM(UVCCM) Mkoa wa Mbeya, Yona Sonelo, akimpa kongole, Kamanda wa UVCCM wilaya ya Mbeya Vijijini, Oran Manase Njeza, baada ya kuapishwa.
Kushoto ni Meya wa Ilala Jijini Dar es Salam, Jerry Silaa, baada ya kiapo cha makamanda wa UVCCM Mkoa na wilaya tisa za mkoa huo. Kulia ni kamanda wa wilaya ya Chunya, Phillip Mullugo.
Kutoka kushoto ni katibu wa idara ya Hamasa na chipukizi Taifa, Paul Makonda, kamanda wa Jumuiya ya Vijana wa CCM(UVCCM) Mkoa wa Mbeya, Yona Sonelo, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mbeya, Aman Kajuna na Meya wa Ilala, Jerry Silaa, baada ya kamanda huyo kuapishwa katika viwanja vya Ruanda Nzovwe jana Jijini Mbeya.
Kushoto ni Mmwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mbeya, Amani Kajuna, baada ya kumpatia maua kwa niaba ya kamati ya utekelezaji ya mkoa wa Mbeya2014, kamanda wa Jumuiya ya Vijana wa CCM(UVCCM) Mkoa wa Mbeya, Yona Sonelo, baada ya kuapishwa jana viwanja vya CCM ILOMBA Jijini Mbeya.
Katikati ni kamanda wa Jumuiya ya Vijana wa CCM(UVCCM) Mkoa wa Mbeya, Yona Sonelo, akisoma kiapo cha ukamanda.
Aliyekuwa Katibu wa CHADEMA Kata ya Iyunga Mbeya, akisema sasa yupo huru, na kuhamia CCM.
Kushoto ni Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa akihesabu fedha ili apatiwe msanii wa nyimbo za asili mkoani Mbeya(Awilo) kulia. Katikati ni Meya wa Ilala Jerry Silaa, wakati wa zoezi la kumwapisha kamanda wa UVCCM Mkoa wa Mbeya jana Jijini Mbeya.
Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Mbeya, Godfrey Zambi, akionesha kwa wananchi Dollar 100 ambayo alimpatia msanii wa nyimbo za asili mkoa ni Mbeya jana, katika viwanja vya CCM ILOMBA Jijini Mbeya.
Kushoto ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mbeya, Aman Kajuna na Katibu wake, Said Yasin, wakiwa katika viwanja vya CCM ILOMBA jana, wakati wa sherehe zakuwaapisha makamanda wa umoja huo.
Kulia ni Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, akipewa taarifa kuwa atasimamia na kutekeleza risala ya vijana wanaotakiwa kuinuka kiuchumi Jijini Mbeya.
Kulia ni Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa,akisema neno.
BABY TOT BAND, wapewa hundi ya 500,000 na JERRY SILAA.
Katikati ni Bashir Madodi, kulia ni Mwakiteleke na kushoto ni Charles Mwakipesile.
Kushoto ni kamanda wa UVCCM wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya, Ibrahim Manjilinji, akiwa na katibu mwenezi wa CCM wilayani humo.
*Risala za
Urais zatawala baraza la UVCCM Mbeya
Na Gordon
Kalulunga. Mbeya
KATIBU wa siasa
na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), mkoa wa Mbeya, Bashiru Salum Madodi,
amesema kuwa tatizo kubwa la baadhi ya vijana wa chama hicho(UVCCM), wanatumika
vibaya na wagombea na kukisemea chama bila utaratibu.
Hayo
aliyasema jana katika ukumbi wa CCM mkoa wa Mbeya, wakati wa Baraza kuu la
UVCCM Mkoani hapa, ambalo limefanyika kwa mujibu wa kanuni za umoja huo kwa ajili ya
maandalizi ya kumwapisha kamanda wa Vijana hao mkoa wa Mbeya, Yona Sonelo na
makamanda wa wilaya zote tisa za mkoa huo.
Huku
akitafsiriwa kama anamjibu Katibu wa hamasa wa UVCCM Taifa, Paul Makonda,
ambaye hivi karibuni ametoa tamko kuwa Waziri Mkuu aliyejiuzuru, Edward Lowassa
kuwa hafai kuwania nafasi ya Rais wa Tanzania, alisema kuwa inashangaza vijana
kuenda mbio na kutoa matamko ambayo yanapaswa yatolewe na vikao vya chama
kwanza.
Alisema
kuwa, vijana wengi wanatembea na wanaotaka madaraka, kutokana na vijana kuwa
ndiyo tegemea la taifa, kwasababu wanaweza kukimbia huku na kule.
“Ni kipindi
kigumu sana kwenu, wakati wetu akina Guninita waliwahi kufutwa uongozi kutokana
na tabia zinazofanana na vijana wa leo. Mnatoa matamko bila hata vikao vya
chama kutoa maamuzi” alisema huku akishangiliwa.
Mjumbe wa
kamati ya utekelezaji ya UVCCM Mkoa wa Mbeya kutoka wilaya ya Momba mkoani
hapa, Hassan Nyalile, alimwambia mwandishi wa mtandao huu kuwa, anaunga mkono kauli ya
Madodi na kusema kuwa kauli aliyoitoa ni ya kiungozi na kwamba Makonda
anatakiwa kujirekebisha na kurudi kwenye majukumu yake.
“Makonda
anatakiwa atafsiri vema kauli ya Madodi na kurejea kwenye misingi ya kanuni ili
aweze kufanya vema kazi za jumuiya yake ya watoto badala ya kila wakati kuinuka
na kutoa matamko ambayo yanaashiria yupo na kiongozi mmoja mfukoni kutafuta
nafasi ya Rais mwaka 2015”
Kwa upande
wake, Paul Makonda ambaye alikuwepo kwenye Baraza hilo, ndiye aliyeanza kueleza
kuwa vijana wapo ndani ya mifuko ya wanasiasa wakubwa, ndiyo maana inafiia
mahala chama hakiwaamini.
Alisisitiza
kuwa, kuna baadhi wanaomtuhumu kuwa yeye anatumwa na kundi la watu kutoa
matamko, jambo ambalo siyo la kweli bali anaongozwa na akili zake mwenyewe na
madhara ya magenge ni kujitafutia riziki binafsi.
Mwenyekiti
wa UVCCM Mkoa wa Mbeya, Amani Kajuna, alisema kuwa vijana wangoje chama kitoe
maamuzi kwanza ya mgombea nafasi ya Urais ndipo vijana wamuunge mkono mtu huyo,
badala ya kugawanyika kwa sasa.
Mgeni rasmi
katika ufunguzi wa Baraza hilo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, ambaye pia ni
Naibu Waziri wa Kilimo chakula na ushirika, Godfrey Zambi, alisisitiza umoja
miongozi mwa Jumuiya hiyo ya vijana kwa maslahi ya chama na Taifa.
Aliipongeza
kamati ya utekelezaji ya UVCCM Mkoa wa Mbeya, kwa kuendeleza kudumisha muungano
kwa kuwaalika viongozi wengine wa umoja huo kutoka mikoa mingine ya Tanzania
Bara na Zanzibar.
“Si vibaya
ili kuendelea kudumisha muungano kuendelea kuoleana alisema Zambi.
Katika hatua
nyingine Zambi amekemea vikali tabia ya makatibu wa chama hicho kuhodhi magari
ya chama kwa kufanya kazi zao binafsi badala ya kazi ya chama kama
ilivyokusudiwa.
Zambi
alisema magari hayo yamenunuliwa mahususi kwa ajili ya kufanya uhamasishaji si
kwa chama tu bali hata jumuiya zote ndani ya chama zinapokuwa na kazi ya
kufanya basi gari hiyo itumike.
“Nawaagiza
makabitu wote kuacha tabia ya kutumia magari haya katika kazi zao binafsi kama
kwenda harusini,kanisani,sokoni ili hali kuna shughuli za chama,vijana iwapo
mtanyimwa gari na katibu yeyote kwa shughuli ya chama nipigieni simu mimi moja
kwa moja,”alisisitiza.
Post a Comment