Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAMA ALIYEMUUA 'MWANAYE' APANDISHWA KIZIMBANI

               

Amina Ibrahim (27), mkazi wa Kimara jijini Dar anayeshikiliwa kwa kesi ya kumuua 'mwanaye'.
MKAZI wa Kimara Amina Ibrahim (27), amepandishwa Kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni Jijini Dar es Salaam akikabiliwa na shitaka la kumuua mtoto wa kambo.

Akisomewa kosa hilo leo mbele ya Hakimu Amalia Mushi, Wakili wa Serikali Faustine Sylivester, alidai kuwa tukio hilo lilitokea Juni 18 mwaka huu huko Kimara, Wilayani hapo.
Sylivester alidai kuwa mshitakiwa alikuwa akiishi naye na ndipo alipoamua kumuua mtoto huyo ajulikanaye kwa jina la Munir Dodi (6), wakati akifahamu kuwa kufanya hivyo ni kosa la jinai kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mshtakiwa hakutakiwa kujibu kitu chochote kutokana na kosa lake kwani Mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo, hivyo kesi imeahirishwa hadi Agosti 15 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.
KUJUA ZAIDI JUU YA HABARI HII, INGIA HAPA: MADAI MAZITO MAMA AMUUA MTOTO

                GPL
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top