Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MBINU MPYA ZA KUWABANA WANAOKWEPA KUREJESHA MIKOPO ZAANIKWA

 

Serikali imetangaza kuwa haitawaruhusu wahitimu wa elimu ya juu wanaodaiwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) kwenda nje ya nchi kwa masomo zaidi au kufanya kazi mpaka watakapomaliza kulipa madeni yao.
Akizungumza bungeni hivi karibuni, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jenista Mhagama alisema hatua hiyo inalenga kuongeza kiwango cha ukusanyaji wa mikopo ambayo imeshawanufaisha wahitimu wengi ingawa ni wachache wanaorejesha.
"Tumezungumza na idara ya uhamiaji ili wale wote wanaotaka kwenda kufanya kazi nje ya nchi wasiruhusiwe mpaka watakapomaliza kulipa mikopo yao ya elimu ya juu. Lengo ni kuepuka ukwepaji unaojitokeza baada ya kuajiriwa," alisema.
Suala la wahitimu wa Kitanzania kutafuta kazi nje ya nchi limekuwa likizungumzwa na wadau wengi kama njia mbadala ya kupata ajira, kutokana na kuwapo kwa ushindani mkubwa wa soko la ndani la ajira.
Wahitimu
Hata hivyo, baadhi ya wadau hawaoni manufaa endelevu ya mpango huo, wakisema chombo kinachohusika na mikopo hakijajipanga vilivyo kukusanya madeni na ndiyo maana kimeshindwa kuwafikia hata wadaiwa waliomo nchini.
Leonard Mhongole ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Ardhi mwaka 2010. Anasema mkakati huo hauwezi kuleta tija kwa kuwa ni watu wachache sana wanaofikiria kwenda nje ya nchi.
"Mamlaka husika zinaangalia sana waajiriwa wa serikalini lakini kwa wale tunaofanya kazi sekta binafsi au waliojiajiri hatufikiwi. Kama watu wote watabanwa kama inavyotakiwa nadhani fedha za kutosha zitarudi serikalini," anasema na kuongeza:
"Mimi binafsi nilitakiwa niwe nimeanza kulipa mkopo wangu lakini kwa kuwa hakuna anayenitaka kufanya hivyo siwezi kuwatafuta wahusika...inawezekana wametoa msamaha kwa baadhi ya watu."
Kwa upande wake, mwanafunzi wa shahada ya uzamili katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Joseph Isindikiro, anas
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top