Na Mwandishi wetu
Mbunge
wa Kigoma kusini David Kafulila amehojiwa na kuwasilisha ushahidi wake
kwa maandishi kuhusu suala la tuhuma za wizi katika akaunti ya Tegeta
Escrow huku akieleza sababu zake ni kwanini anataka Bunge lichunguze
badala ya mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali na Takukuru
Kafulila
ametoa andiko la kurasa saba kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru
huku nakala zikitolewa kwa Spika wa Bunge na Mkaguzi na mdhibiti wa
hesabu za Serikali, ametoa maelezo akiambatanisha na vielelezo kadhaa
juu ya tuhuma hizo.
“Nikichangia
hotuba ya Waziri mkuu nilitaka uchunguzi ufanyike kupitia kamati teule
ya bunge kuhusu tuhuma zinazohusisha kiasi cha dola 270 Milion
zilizopaswa kuwa ndani ya akaunti hiyo sanjari na zile dola 122 milion
zilizokwishatolewa na kupewa kampuni ya PAP inayomilikiwa na
mfanyabiashara” ilisema sehemu ya maelezo hayo.
Kafulila
amesema ni kwasababu Takukuru ni chombo chenye jukumu zito lakini haina
meno kukabiliana na rushwa zinazowakabili vigogo wa serikali kwani
mwamuzi wa mwisho katika masuala hayo huwa ni ofisi ya DPP ambaye
amekuwa akitupilia mbali mashtaka kwa kisingizio cha mamlaka aliyonayo
kikatiba.
Kwa
mujibu wa barua hiyo ni Malalamiko ya Ofisi ya Takukuru yenyewe kusema
kuwa ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini inakwamisha ufanisi
wa vita dhidi ya rushwa ilikuwa ni ushahidi tosha wa yeye kukataa
uchunguzi ufanywe na Takukuru.
Post a Comment