Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mbunge wa Jimbo la Bunda (CCM), Stephen Wassira ametangaza kuwa atatetea tena nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu ujao


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) na Mbunge wa Bunda-CCM Stephen Wassira
---
 Mbunge wa Jimbo la Bunda (CCM), Stephen Wassira ametangaza kuwa atatetea tena nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu ujao, huku akijigamba kuwa yeye ni “mwarobaini wa matatizo” yanayowakabili wakazi wa jimbo hilo.
Kabla ya kutangaza nia hiyo jana, mara kadhaa Wassira amekuwa akihusishwa na suala la urais na ni mmoja wa makada sita wa CCM ambao walipewa adhabu na chama hicho, Februari 18, mwaka huu baada ya kukutwa na makosa ya kuanza mapema kampeni za urais mwaka 2015.
Wassira, ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) alitangaza uamuzi wake huo katika kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM wilayani Bunda kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya hiyo.

Wassira, ambaye ana umri wa miaka 69, aliwaponda wanaombeza kuwa amezeeka, hivyo kuweka wazi kwamba ameamua kuwania tena nafasi hiyo kwa sababu bado ana nguvu na uwezo wa kuwatumikia wananchi kwa kipindi kingine cha miaka mitano na kutimiza ndoto zao za kupata maisha bora kwa kila mmoja wao.

“Ndugu wajumbe napenda kutumia nafasi hii kutangaza rasmi kwamba ninagombea tena ubunge wa jimbo hili. Wale wanaokereka wakereke tu. Nina nguvu bado za kuwatumikia Wanabunda,”alisema Wassira.
“Nyote ni mashahidi kwa jinsi ninavyoshirikiana nanyi katika kuondoa changamoto zinazotukabili ambazo nyingi ziko karibu kuisha ili wote wapate maisha bora yaliyoahidiwa na CCM. Nawaombeni tu tuzidi kushirikiana,” alisema Wassira, ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM.Kwa habari Zaidi Bofya na Endelea.......
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top