Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MSANII TUNDA MAN APIGIWA NA KUPOKEA SIMU YA AJABU

 

Kuna kipindi stori za namba ambazo wengi walikua wakisema za ajabu na endapo zikikupigia usipokee zilikuwa zikitawala sana kwenye mitandao ya kijamii na wengi pia walikua wakizonyesha namba hizo. 
 
Tunda Man ambaye pia ni miongoni mwa watu wanaounda kundi la Tip Top Connection Jioni ya July 28 amepata simu hiyo ambayo amedai kwake ilikua ni mara ya kwanza kupigiwa kwani namba hizo hajawahi kuziona zikimpigia kabla.
2ndaTunda man ameongea  na kusema>>’Nilikua nafuturu jana jioni wakati naendelea kufuturu nikapigiwa simu namba sikua nazijua kwani zilikua za maajabu tu,sikupokea,ilipiga kama mara 30 hivi’
 
‘Baadae nikapokea na kisha nikaiweka mbali kidogo na mimi wakati nasema hallow ghafla kitu kama shoti ya umeme kikaanza kutembea kwenye viganja mpaka kwenye mkono nikakosa nguvu kabisa nikawaambia jamani nipelekeni hospital’
‘Tukaenda hospital ya Serikali hapo Palestina,Dokta akasema huu ugonjwa tangu ameanza kutibia watu hajakutana nao ni mara yake ya kwanza hivyo matibabu aliyokuwa akinipatia ni kama ya mtu aliyepooza ghafla’
‘Kwa sasa namshukuru Mungu naendelea vizuri ingawa kuna dawa nimepewa zingine nameza mara 2 kwa siku na vidonge vingine ni mara 3 kwa siku pia nimechomwa sindano’
Hii ndiyo namba iliyompigia Tunda
12nda 
na millardayo.com
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top