Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MTOTO WA MIEZI MINNE ATEKETEA KWA MOTO MKOANI NJOMBE

 


Mtoto Mwenye Umri wa Miezi Minne Celin Kyando Amefariki  Dunia Baada ya Chumba Alichokuwa Amelala Kuteketea na Moto Katika Mtaa wa Buguruni Mjini Njombe Wakati Mama Yake  Rose Luambano Akiwa Bafuni Anaoga.
 
Mtandao huu Umefika Eneo la Tukio na Kuzungumza na Baadhi ya Mashuhuda Ambao Wamesema Kuwa  Tukio Hilo Limetokea Majira ya Saa Sita Mchana Julai Sita Mwaka Huu na Kuongeza Kuwa Chanzo cha Ajali Hiyo ya Moto ni kifaa cha umeme kitumikacho kupashia maji (Hita) ambayo iliachwa bila ya kuzimwa.

Hati Hivyo Mashuhuda Hao Kwa Kushirikiana na Wananchi wa Mtaa wa Buguruni Wamefanikiwa Kuzima Moto Huo Kabla ya Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Pamoja na Jeshi la Polisi Kufika Eneo la Tukio , Huku Baadhi ya Wapangaji Wengine wa Nyumba Hiyo wenye maduka  Wakionekana Kuhamisha Mali Zao Kwa Hofu ya Kuungua.
 
Tukio hilo lililotokea kwenye Nyumba ya Bw. Danfoard Mhelela yenye Namba za Usajili MTW 94 ambapo Licha ya kufariki dunia kwa mtoto huyo lakini pia vitu mbalimbali vimeteketea kwa moto.
 
Wameleza  Kuwa Baada ya Jeshi la Polisi Kufika Eneo la Tukio Limeuchukua Mwili wa Mtoto Huyo Pamoja na Wazazi Wake na Viongozi wa Mtaa Huu na jududi za kupata uthibitisho kutoka kwa jeshi la polisi bado zinaendelea.

Mwenyezi mungu ailaze roho ya mtoto celin mahala pema peponi.
 
Na  James Festo, hfesto blog Njombe.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top