Ndugu zangu,
Uafrika
ni imani. Uafrika umejijenga katika upendo na ujamaa. Ndio maana Mwalimu
aliijenga TANU na nchi yetu katika misingi ya Ujamaa wa Kiafrika, hivyo
basi itikadi. Ni tofauti kabisa na Ukomunisti.
Mathalan,
Afrika unapokuwa safarini na jua likazama, basi, Mwafrika hutafuta
yalipo makazi ya watu. Afrika safari zetu nyingi ni za miguu, na kwa
kawaida hatutembei usiku.
Na jua
likizama na ukakutana na Mwafrika mwenzako kwenye mji wake, husemi kuwa
unataka kusaidiwa pa kulala na mengineyo. Kwa mila zetu, utasema; "
Mwenzenu niko safarini na jua limezama nikiwa hapa".
Kwa
Mwafrika, hapo umehitaji msaada. Mwenyeji ataandaa pa wewe kulala.
Utaandaliwa chakula na hata maji ya moto ya kuoga. Atakayefanya ukarimu
huo hatajali kama wewe ni Mkristo, Muislamu, au wa kabila tofauti na
yeye.
Na asubuhi kukipambazuka, utapewa kijana wa kukusindikiza kilomita zipatazo mbili. Uendelee na safari yako.
Na asubuhi kukipambazuka, utapewa kijana wa kukusindikiza kilomita zipatazo mbili. Uendelee na safari yako.
Ndio, Uafrika ni imani iliyojengeka katika misingi ya upendo, umoja na kusaidiana bila kubaguana.
Ni Neno Fupi La Leo
Maggid Mjengwa,
Iringa.
Ni Neno Fupi La Leo
Maggid Mjengwa,
Iringa.
Post a Comment