Na Baraka Mbolembole
Uholanzi ilifuzu kwa mara ya pili
mfululizo nusu fainali ya kombe la dunia baada ya kuwashinda timu ya
Costa Rica kwa changamoto ya mikwaju ya penalti dhidi ya Costa Rica
katika mchezo pekee wa robo fainali ambao ulichezwa kwa dakika 120 na
matokeo kuwa suluhu-tasa.
Sasa ‘ wataalamu wa soka la
mbinu’ Ujerumani na Uholanzi watakutana na timu zenye vipaji kutoka ‘
bara la soka’. Kwa mara ya kwanza timu za Brazil na Argentina zimefuzu
kwa wakati mmoja hatua ya nusu fainali na mafanikio yametokana na timu
hizo kucheza kwa ushirikiano na umakini mkubwa katika michezo mitano
iliyopita.
UJERUMANI vs BRAZIL
Ujerumani waliichapa Ureno kwa
mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza, baada ya hapo kikosi cha Joachim Loew
kimemuda kufunga mabao sita katika michezo minne iliyopita, watacheza
na wenyeji, Brazil katika mchezo wa nusu fainali , jumanne hii. Mchezo
huo unataraji kuwa mgumu lakini bado safu ya ulinzi ya kikosi cha
Ujerumani kinatakiwa kupunguza utegemezi kutoka kwa golikipa, Manuel
Neur ambaye alifanya kazi kubwa katika mchezo wa robo fainali dhidi
Ufaransa pale alipookoa nafasi za wazi.
Neur anafanya vizuri kazi yake
hadi sasa kama golikipa ni lazima afanye vyovyote vile kuhakikisha mpira
hauingii golini. Ila, kitendo chake cha kuingia katika majukumu ya
ulinzi wa kati katika mchezo dhidi ya Algeria wa hatua ya 16 bora ni
kielelezo tosha kuwa safu hiyo ya ulinzi ya ‘ National Eleven’ inapitika
kiurahisi pale wanaposhambulia. Low alimuondoa mlinzi, Per Mertesacker
na kuwapanga, Mat Hummels na Benedkt Howes katika mchezo wa robo
fainali. Hummels alifunga bao pekee katika mchezo huo akiunganisha kwa
kichwa mpira wa faulo uliopigwa na Ton Kros, alitajwa kama mchezaji bora
wa mechi kutokana na kucheza kama kiongozi wa idara ya ulinzi na
kulinda bao hilo kwa dakika 81.. Pamoja na tuzo hiyo kupewa Hummels,
golipika, Neur alifanya kazi kubwa kuokoa michomo ya Karim Benzema
Rafu mbaya iliyochezwa na mlinzi
wa Colombia, Juan Zuniga dakika ya 88 imemuondoa Neymar katika michuano
japo timnu yake ilifanikiwa kjufuzu kwa mchezo wa nusu fainali. Neymar
hatukuwepo katika mchezo dhidi ya Ujerumani siku ya jumanne ijayo, na
hatoweza kushiriki katika mchezo wa fainali, julai 13 endapo Brazil
itafanikiwa itafanikiwa kufika fainali ya michuano hiyo ya 20. Staa huyo
wa Brazil alikuwa kila kitu kwa timu yake katika michezo mitano
iliyopita , na alicheza huku akizunguka eneo lote la mashambulizi la
Colombia, hakika Brazil itamkosa mchezaji muhimu sana lakini bado
mhistoria inawabeba mbele ya Ujerumani, mabingwa mara tatu wa michuano
hiyo.
Nahodha na mfungaji wa bao la
kwanza la Brazil dhidi ya Brazil, Thiago Silva hatokuwepo katika mchezo
ujao kutokana na kupata kadi ya pili ya njano katika mchezo huo
walioibuka na ushindi wa mabao 2-1. Kocha wa Selecao atakuwa katika
mtihani wake mkubwa zaidi kabla ya kushinda taji lake la pili wakati
Brazil itakapokuna na timu iliyocheza mchezo wa nidhamu kubwa na
kujilinda katika muda mwingi wa mchezo wa robo fainali dhidi ya
Ufaransa.
Ujerumani imefuzu nusu fainali
yake ya nne mfululizo na kuwa timu ya kwanza kufanya hivyo, itakuwa
ikiweka rekodi nyingine ya michuano ya timu iliyocheza michezo mingi
zaidi mfululizo ya michuano hiyo. Mchezo dhidi ya Brazil utakuwa ni wa
27 hivyo watakuwa wakivunja rekodi ya Brazil ambao walicheza michezo 26
mfululizo ya michuano hiyo. Selecao ilicheza michezo yote saba ya
michuano kuanzia fainali za mwaka 1994, 1998, 2002 na waliishia robo
fainali mwaka 2006 walipofungwa na Ufaransa, timu ambayo safari hii
imeshindwa kuwazuia Ujerumani baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0.
Scorali atakuwa katika mtihani mkubwa katika kufanya machaguo ya
wachezaji wa kuanza katika mchezo dhidi ya ‘ National Eleven’.
Adriano Leite alifunga bao la
kuongoza kwa Brazil katika dakika ya 21, Lukas Podolski akasawzisha
dakika mbili baadae na kufanya matokeo kuwa bao 1-1. Dakika ya 43,
Ronaldinho Gaucho akafunga bao la pili kwa mkwaju wa panalti, dakika
mbili baadae nahodha wa zamani wa Ujerumani, Michael Ballack
akasawazisha kwa njia ya penalti na kufanya timu hizo kuwa sare ya mabao
2-2 katika nusu ya kwanza ya mchezo wa nusu fainali wa kombe la
Mabingwa wa Mabara, juni, 25, 2005,jijini Berlin. Ushindi huo ni wa
mwisho kwa Brazil dhidi ya Ujerumani katika kipindi cha muongo mmoja
sasa.
Ushindi wa mabao 3-2 katika
mchezo wa kimataifa wa kirafiki ambao Ujerumani iliupata, agosti, 2011
ndiyo pekee ambao wamewahi kuupata katika kipindi cha miaka 14
iliyopita. Wakati mchezo wa mabingwa wa mabara ulitoa mabao manne katika
kipindi cha kwanza tu huku mikwaju miwili ya penalti ikitumika, katika
mchezo mabao yote matano yalifungwa katika muda wa dakika 30 za mwisho.
Kiungo Bastian Schweinsteiger alifunga bao la kuongoza kwa njia ya
mkwaju wa penalti, Mario Gotze akaoneza bao lingine dakika sita baadae.
Robinho alifunga bao la kwanza la
Brazil kwa njia ya penalti katika dakika 71, kabla ya Andre Schurrle
kufunga bao la tatu dakika ya 80 na kufanya Ujerumani kuongoza kwa mabao
3-1. Neymar alifunga bao la pili la Selecao katika dakika ya mwisho ya
mchezo huo uliomalizika kwa Brazil kulazwa mabao 3-2. Mchezo pekee ambao
ulimalizika kwa sare baina ya timu hizo ni ule wa , septemba, 2004
wakati, mshambulizi, Kelvin Kuranyi aliposawazisha katika dakika ya 17
akifuta bao la mepema dakika ya tisa lililofungwa na Gaucho. Mchezo huo
ulimalizika kwa sare ya kufunga bao 1-1.
BRAZIL INAITESA UJERUMANI KATIKA KOMBE LA DUNIA
Ujerumani walicheza kwa kujiamini
dhidi ya Ufaransa hata pale walipokuwa katika wakati mgumu hiyo ndiyo
tabia alisi ya wachezaji wa Ujerumani kizazi hadi kizazi . Wachezaji wan
chi hiyo wamekuwa wakiongozwa na historia nzuri ya vikosi vilivyopita
na wameendeleza hilo katika fainali zinazoendelea nchini Brazil.. Kocha
Loew aliamua kumuacha nje mlinzi wa Arsenal, Per Mertesacker na kumpanga
Benedikt Howes kutoka na Per kutokuwa na kasai na udhaifu huo
uliwafanya kupata shida katika mchezo wa hatua ya 16 bora dhidi ya
Algeria.
David Luiz alifunga ‘ bao la
nguvu na la aina yake’ atamkosa patna wake Silva lakini nafasi hiyo
inataraji kuzibwa na mlinzi wa Bayern Munich, Dante ambaye hajacheza
mchezo wowote katika michuano. Nafasi hiyo inaweza kuzibwa lakini ‘ Big
Phill’ atalazimika kufanya mabadiliko katika safu ya mashambulizi kwa
kuwas amempoteza mchezaji wake bora zaidi kikosini, Neymar. Brazil
inaweza kubebwa na mshambulizi, Hulk ambaye amekuwa akitumika zaidi kama
kiungo wa mashambulizi akitokea pembeni. Hulk ni mshambulizi na
mfungaji mahiri wa kati, ila kiwango cha chini ambacho kimeendelea
kuoneshwa na Fred ni tatizi kubwa kwa Brazil kwa kuwa JO, mshambulizi
mwingine wa nyongeza katika kikosi hana kasi na ‘ mlaini’ sana.
Timu hizo zimewahi kukutana mara
moja katika michezo ya kombe la dunia. Brazil ilitwaa ubingwa wake wa
mwisho wa dunia mwaka 2002 baada ya kuichapa Ujerumani kwa mabao 2-0
yaliyofungwa na Ronaldo De Lima katika uwanja wa Yokohama, Japan. Baada
ya hapo kikosi hicho kimefundishwa na makocha wqatatu tofauti, Carlos
Alberto Perreira ambaye aliipeleka timu hiyo hadi katika robo fainali
katika fainali za mwaka 2006, na chini ya Carlos Dunga timu hiyo
iliishia tena robo fainali katika fainali za mwaka 2010. Baada ya
kuondoka, Dunga, Selecao ilimpata mwalimu, Mano Menezes ambaye aliingoza
timu hiyo kwa miaka mitatu kabla ya kumuachia, Scorali mapema mwaka
jana.
Ujerumani imekuwa chini ya
Joachim Loew tangu mwaka 2006, lakini mwalimu huyo alikuwa msaidizi wa
Jurgen Klinsmann kwa miaka miwili kabla ya kupewas mikoba rasmi ya
kuinoa timu hiyo. Loew amekuwa sehemu ya kombe la dunia katika michuano
miwili iliyopita na mara zote alishuhudia kikosi cha kikiondoshwa katika
nusu fainali. Mwaka 2006 walipokuwa wenyeji walifungwa pasipo
kutarajiwa na Italia, na mwaka 2010 walifungwa na Hispania na timu zote
hizo zilifanikiwa kutwaa taji katika michezo ya fainali.
Brazil haijawahi kupoteza mchezo
wa nusu fainali wa kombe la dunia, wakati Ujerumani imepoteza mara nne.
Kipa wa Ujerumani, Manuel Neur aliokoa nafasi tano za wazi katika
mchezo war obo fainali dhidi ya Ufaransa katika mchezo ambao safu yake
ya ulinzi ilipokea mashambulizi 13 huku mipira tisa ya hatari ikifika
langoni. Timu ambayo ilianza michuano kwa kuitandika Ureno mabao 4-0
ilishambulia mara nane tu huku mashambulizi sita yakiwa ya uhakika.
Ujerumani imeendelea kuwa timu ya michuano na itawabidi kugangamara hasa
ili kuvuka hatua ya nusu fainali mbele ya Brazil ambao wamefunga mabao
kumi katika michezo mitano iliyopita.
Wakati kikosi cha Loew kilicheza
faulo 18 na wachezaji wake wawili kuonyeshwa kadi za njano, Selecao
ilikuwa na siku nzuri japo ilishuhudia mshambulizi wake namba moja
akiumia dakika mbili kabla ya kumalizika kwa mchezo war obo fainali.
Brazil imekuwa timu yenye nguvu katikati ya uwanja na katika safu ya
nyuma. Ikiwa imeruhusu mabao matatu hadi sasa, timu hiyo ilicheza faulo
mara 31 huku wakipokea mashambulizi mara 11. Itampokea tena kiungo wake
wa ulinzi, Luis Gustavo ambaye alikuwa akitumikia kadi katika mchezo war
obo fainali. Tofauti na Ujerumani ambao walimiki mpira kwa asilimia
sawa na Ufaransa-50+50, vijana wa Big Phill walimiki mpira kwa asilimia
moja zaidi ya timu ambayo ilikuwa ikiogopewa sana katika michuano ya
mwaka huu.
0714 08 43 08
Imechotwa: shaffihdauda.com
Post a Comment