Baadhi ya watumiaji wa mtandao wa Facebook wameanzisha kampeni kubwa
kuitaka kampuni hiyo kuondoa picha za binti mdogo mwindaji anayeonekana
amepiga picha na wanyama wakali anaodai kuwaua katika nchi za kiafrika
ikiwemo Zimbabwe.
Binti huyo Kendall Jones kutoka Cleburne, Texas, anadaiwa kuwa ni
mwindaji mdogo zaidi kuwapiga risasi wanyama hao wakali wa mwituni
akiwemo Chui na kuthibitisha hilo amekuwa akipozi nao kwa picha baada ya
kufanya kitendo hicho.
Maelfu ya watu wanaitaka Facebook kuondoa picha hizo ambapo binti huyo amejitetea kuwa anafurahi kuendeleza ndoto zake.
Lakini
pia binti huyo ameandika kupitia akaunti yake ya Facebook kuwa
anatarajia kuanzisha kipindi chake cha Televisheni ifikapo mwaka 2015.
Binti huyo amekuwa akitabasamu na kuweka pozi pembeni ya wanyama wa
aina mbalimbali anaodai kuwaua ambapo picha hizo zimeamsha hisia kali
katika mitandao ya kijamii watu wakidai ziondolewa.
Mmoja wa mashabiki amenukuliwa akisema kuwa”Kwa vyovyote vile
utakavyoangalia, kuona mtu anatabasamu pembeni ya mwili uliokufa ni
kitendo cha kuhuzunisha sana.”
Post a Comment