Uongozi wa Palestina umependekeza makubaliano ya saa ishirini na nne ya kusitisha mapigano dhidi yake na Israel.
Yasser
Abed Rabbo wa chama cha PLO, Palestine Liberation Organisation amesema
mpango huo umeungwa mkono na makundi muhimu likiwemo kundi la Hamas na
la Islamic Jihad.
Hata hivyo mmoja wa maafisa wa Hamas Abu Zuhri amesema taarifa hiyo ya PLO haiwakilishi upande wa Hamas.
Mapema
pendekezo la makubaliano ya kusitisha mapigano lililotangazwa,
halikuweza kutekelezwa kwa kuwa hakuna upande wowote ulioweza
kulitekeleza kwa kusitisha mapigano katika eneo la Gaza.
Bwana
Rabbo amesema ujumbe wa pamoja unaoongozwa na Rais wa Palestina Mahmoud
Abbas utakwenda Cairo kuweka masharti ya kusitisha mapigano.CHANZO BBC
SWAHILI
Post a Comment