Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi |
Na Emanuel Madafa,Mbeya
Mwanamke mmoja Mkazi wa kijiji cha Mkutano Ndugu
Mariana Simtowe (32) anashikiliwa na
jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa tuhuma za kumuuwa mume wake Ndugu Petro Mteka (33) Mkazi wa kijiji cha
mkutano kwa kumpiga kwa kipande cha mti.
Tukio hilo limetokea Julai 13mwaka huu majira ya saa 21:00 usiku huko katika kijiji
cha mkutano. Kata ya Nzoka, wilayani ya Momba, Mkoa wa Mbeya.
Inadaiwa kuwa mtuhumiwa akiwa njiani na marehemu mume
wake wakitokea kilabu cha pombe za kienyeji wakiwa wamelewa ilitokea hali ya
kutoelewana [ugomvi) na ndipo mtuhumiwa alipo tumia kipande cha mti na kumpiga
nacho mume wake na kumsababishia majeraha.
Kutokana na majeraha aliyokuwa ameyapata mwanaume
huyo, alipelekwa katika zahanati ya kijiji cha mkutano kwa matibabu na
alifariki dunia mnamo tarehe 14.07.2014 majira ya saa 09:00 asubuhi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina Msaidizi
mwandamizi wa Polisi Ahmed z. Msangi
anatoa wito kwa jamii kuacha tabia ya unywaji wa pombe kupita kiasi kwani ni
hatari kwa afya zao na huleta madhara katika jamii.
Aidha anatoa wito kwa wana ndoa kutatua migogoro yao
kwa njia ya kukaa meza moja ya mazungumzo ili kupata muafaka.
MWISHO
Post a Comment